2025
Baki Umeunganishwa na Mwokozi
Machi 2025


“Baki Umeunganishwa na Mwokozi,” Liahona, Machi 2025.

Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Baki Umeunganishwa na Mwokozi

Tulipoanza kushuka kutoka kileleni, ghafla baba na dada yangu walitupwa nje ya gari lao!

watu wawili katika mavazi ya michezo wamesimama kwenye barabara ya matope, na ATV iliyopinduliwa karibu

Kielelezo na David Miles

Majira ya joto familia yangu ilikwenda likizo kusini mwa China, ambapo tuliendesha magari yote ya mandhari ya nchi (ATV) kupitia misitu ya mvua. Tulipofika kwenye kambi ya ATV, tulishangazwa wakati waongozaji walipotupa suti za ulinzi kamili na helmeti kubwa na miwani. Ilionekana kidogo kwa wasafiri wa ridhaa kwenye siku hiyo ya joto, unyevu, lakini tulivaa mavazi hayo hata hivyo.

Baada ya kupokea maelekezo ya kuendesha gari, tuliondoka na hatimaye kufikia kilele cha safari yetu. Hapo tulisimama ili kunywa maji na kuifuta jasho kutoka kwenye nyuso zetu.

Mwongozaji wetu kisha alielezea kwamba kwenda chini kungekuwa kwa utelezi zaidi. Tungehitaji kukaa karibu pamoja na kuunda treni ya ATV, kwa kila ATV inapogusa chombo mbele yake na nyuma kunaimarisha kundi.

Tulipoanza kushuka, tuliitana sisi kwa sisi kuratibu ushukaji wetu. Taratibu tulitenganishwa, hata hivyo, tukiacha pengo kati ya gari langu na ATV lililoendeshwa na baba yangu na dada yangu mdogo, Vivi. Ghafla Vivi na baba yangu walitupwa nje ya gari lao! Baba yangu aliruka juu ya Vivi wakati tu ili kumlinda kutokana na ATV isimwangukie.

Tulifarijika sana tulipowaona baba yangu na Vivi wakisimama na kukung’uta mavumbi kwenye suruali zao. Shukrani kwa mavaziya kinga waliyovaa, baba yangu alipata majeraha madogo tu. Vivi alishtuka lakini hakujeruhiwa. Tulipokutanika tena kama kikundi, mwongozaji alitukumbusha katika sauti imara kwamba tunapaswa kudumisha muunganiko wa ATV zetu ikiwa hatukutaka kuanguka chini ya mlima tena.

Katika maisha wakati mwingine tunajaribiwa kufikiria tunaweza kufanya mambo sisi wenyewe. Tunafikiri hatuhitaji kuvaa silaha za ulinzi za injili, ambazo zinaweza kutufanya tusijisikie vyema. Vivyo hivyo, tunaweza kuona vigumu wakati mwingine kubaki tumeunganika na Baba yetu wa Mbinguni. Tunaposhindwa kufanya hivyo, tunahatarisha kupitia njia za kuogofya na za kutisha za ulimwengu peke yetu, tunakabiliwa na ajali kali za kiroho na majeraha.

Ikiwa tutatumia ulinzi ambao injili hutoa na kubaki tumeunganishwa na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, tunaweza kukabiliana na changamoto zilizo mbele yetu katika maisha. Bila kujali njia inavyoogopesha au kutisha kiasi gani, pamoja na Wao tunaweza kufanikiwa.