2025
Kuvikwa na Uwezo kutoka Juu
Machi 2025


“Kuvikwa na Uwezo kutoka Juu,” Liahona, Machi 2025.

Mitazamo ya Kihistoria juu ya Nyumba ya Bwana

Kuvikwa na Uwezo kutoka Juu

Kama wanafunzi katika Agano Jipya, Watakatifu wa Siku za Mwisho waliahidiwa endaumenti ya nguvu kutoka kwa Bwana.

Mwokozi mfufuka akiwafundisha wafuasi Wake

Katika majira ya kuchipua ya mwaka 1836, Charles Rich alikuwa mmisionari akihubiri injili ya urejesho huko kusini mwa Ohio. Alilazimika kuvunjika moyo kwamba aliwasili Kirtland, Ohio, mnamo Aprili 12—takribani wiki mbili baada ya kuwekwa wakfu kwa Hekalu la Kirtland.

Alikuwa amesafiri kwa meli ya mvuke katika Mto Ohio na kisha kutembea karibu maili 100 (160 km). Aliona nyumba ya Bwana juu ya kilele cha miti ya asili kwenye mandhari na kuta zake za bluu na paa nyekundu. Lakini alikuwa amechelewa. Alikuwa amekosa uwekaji wakfu, kusanyiko takatifu, na, alifikiria, endaumenti iliyoahidiwa ya nguvu kutoka juu.

Mnamo Septemba 1830, miezi michache tu baada ya Kanisa la urejesho kuanzishwa, Joseph Smith alipokea ufunuo kutoka kwa Yesu Kristo akiwaita waumini wa Kanisa kukusanyika (ona Mafundisho na Maagano 29:7–8). Miezi michache baadaye Bwana alifunua kwa nini. Watakatifu walipaswa “kwenda Ohio,” ambapo, Yesu alitamka, “Nitawapa sheria yangu; na huko mtajaliwa uwezo kutoka juu; na kutoka wakati huo, yeyote nimtakaye kwenda miongoni mwa mataifa yote” (Mafundisho na Maagano 38:32–33; msisitizo umeongezwa). Waumini wa Kanisa ambao walisikia ufunuo huu wangetambua lugha hii kama inatoka katika Agano Jipya.

Wafuasi wa Agano Jipya Walivikwa na Nguvu

Luka 24 huanza katika wakati wa kukata tamaa. Yesu alikuwa amesulubiwa, na kundi la wanafunzi Wake wanawake walikuwa wamerudi kwenye kaburi Lake. Waligundua kwamba mlango wa jiwe ulikuwa umeviringishwa mbali, na wao “hawakuuona mwili wa Bwana Yesu” (mstari wa 3). Punde wajumbe wa kimalaika waliwapa matumaini: “Hayupo hapa, amefufuka” (mstari wa 6).

Baadaye, Bwana mfufuka aliwatokea wanafunzi Wake na kuwahudumia. Yeye aliwapa kile Wakristo ulimwenguni kote wanatambua kama “Agizo Kuu” la kuhubiri injili ya Yesu Kristo. Yesu alielezea kwamba toba na ondoleo la dhambi linapaswa kuhubiriwa katika jina Lake miongoni mwa mataifa yote (mstari wa 47).

Hata hivyo, Yeye aliwaagiza wanafunzi Wake wasiondoke mara moja: “Kaeni katika mji wa Yerusalemu, hadi mtakapovikwa kwa uwezo utokao juu” (mstari wa 49). Edued (au “endowed” katika Kiingereza cha kisasa) ni tafsiri ya neno la Kiyunani linalomaanisha “kuvikwa nguo.” Wafuasi wa kale wa Kristo walipaswa kusubiri katika Yerusalemu hadi walipovikwa nguvu kutoka juu. Kisha walipaswa kujenga ufalme wa Mungu ulimwenguni kote.

Yesu Kristo akipaa mbinguni

Kabla hajapaa mbinguni, Bwana aliwaambia wanafunzi Wake, “Kaeni katika mji wa Yerusalemu, hata mtakapokuwa mmekwisha kuwa na nguvu kutoka juu” (Luka 24:49).

Watakatifu wa Siku za Mwisho Wamevikwa na Nguvu

Watakatifu wa Siku za Mwisho walikusanyika huko Ohio miaka ya 1830 kwa kusudi kama hilo. Walitazamia “kuvikwa uwezo kutoka juu” (Mafundisho na Maagano 38:32) na kuchukua ujumbe wa Yesu ulimwenguni kote. Hatimaye, Bwana alitamka kwamba Watakatifu hawa “wanapaswa kupokea endaumenti yao kutoka juu ndani ya nyumba yangu” (Mafundisho na Maagano 105:33, msisitizo umeongezwa; ona pia mstari wa 11–12). Bado, wengi wa Watakatifu wa mwanzo hawakujua hasa nini cha kutarajia.

Si muda mrefu baada ya kuitwa na kutawazwa kwa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili mwaka 1835, Joseph Smith alikutana nao kuhusu nyumba ya Bwana. Joseph alitambua kwamba Wale Kumi na Wawili walikuwa “na shauku” na hawakuweza kuelewa kile kilichokuwa kinakuja. Alielezea walihitaji endaumenti ili waweze “kujitayarisha na kuweza kushinda vitu vyote” na kufundisha injili kwa nguvu. “Unapopokea endaumenti,” alieleza, Mitume “watahubiri injili kwa mataifa yote, kabila, na lugha.”

Punde baadaye, Joseph Smith alifunua sherehe zilizopangiliwa kwa mfano wa uwekaji wakfu kwa makuhani wa zamani wa hekalu la Waisraeli. Katika maandalizi ya endaumenti, kila afisa wa ukuhani alioshwa na kupakwa mafuta “kwa aina hiyo hiyo ya mafuta na katika njia ambayo ilikuwa Musa na Haruni, na wale waliosimama mbele za Bwana katika siku za kale.”

Kwa wakati huu, endaumenti ya nguvu ilijumuisha mmiminiko wa nguvu za kiroho wakati wa mkutano maalum wa kusanyiko takatifu. Kama Elijah Able—Sabini mweusi wa kwanza katika Kanisa—maafisa wa ukuhani walifunga, walisali, na kupokea sakramenti ya Karamu ya Bwana kama mlo wa pamoja. Walishuhudia na kutoa unabii, na Mungu aliwabariki kwa kuwapa nguvu. Wale waliopokea endaumenti kisha walitoka kwenda kujenga ufalme wa Mungu kwa kuhubiri injili ya urejesho. Licha ya upinzani, walilindwa katika safari zao, walikuzwa katika mahubiri yao, na kubarikiwa katika familia zao.

Huko Kirtland, ni wanaume pekee walishiriki katika mkutano wa kusanyiko takatifu ambapo walipewa endaumenti kwa uwezo kutoka juu. Hata hivyo, katika miaka michache, Watakatifu walijenga Hekalu la Nauvoo. Hapo Joseph Smith alifunua sherehe zilizopanuliwa za hekalu ambazo ni msingi wa uzoefu wetu wa hekaluni leo. Huko Nauvoo, wanawake vile vile wanaume walivikwa na nguvu.

Akizungumza na akina dada wa Muungano wa Usaidizi, Joseph Smith aliahidi kwamba katika endaumenti ya hekalu “funguo za ufalme” “zingetolewa kwao,” sawa sawa na “kwa Wazee.” Ingawa ingekuwa miongo kadhaa kabla ya wanawake kuitwa kama wamisionari wanaohubiri, wanawake na kazi zao zimekuwa muhimu katika kujenga ufalme wa Mungu duniani.

Ingawa Charles Rich alikuwa amekosa kuwekwa wakfu Hekalu la Kirtland, alijifunza kwamba yeye na wamisionari wengine kadhaa ambao walikuwa wamewasili Kirtland kwa kuchelewa walikuwa wanakwenda kupata uzoefu wa endaumenti. Kwa mfano wa makuhani wa kale wa Waisraeli (ona Kutoka 29; 40), alioshwa na kupakwa mafuta. Alikusanyika pamoja na wengine, kufunga, kusali, na kusherehekea Karamu ya Bwana.

“Tulitoa unabii usiku mzima,” Charles aliandika. “Ilitolewa unabii kwamba wokovu uliandikwa kwenye kila mkono na mguu kiungo na kila kiungo” cha mwili wake. “Nilijazwa na roho ya unabii, na nilivikwa nguvu kutoka juu.”

Alitumia maisha yake yote yaliyosalia—miaka 47—akifanya kazi kama mwanafunzi wa Yesu Kristo, akiujenga ufalme wa Mungu.

Tangu wakati huo, Watakatifu wa Siku za Mwisho kote ulimwenguni wamesafiri kwenda kwenye nyumba ya Bwana ili kuvikwa nguvu kutoka juu. Na kama Watakatifu hawa wa mwanzo, endaumenti inatuandaa kujenga ufalme wa Mungu kama wanafunzi wa Yesu Kristo na siku moja kupokea kuinuliwa kupitia rehema na neema Yake.

Mihutasari

  1. Joseph Smith, “Discourse, 12 November 1835,” 32, 33, josephsmithpapers.org; spelling and punctuation standardized.

  2. Oliver Cowdery, diary, Jan. 21, 1836, Church History Library, Salt Lake City; spelling standardized.

  3. Ona Joseph F. Smith, Notes on Elijah Able, undated [likely ca. 1879], Elijah Able biography, note 5, josephsmithpapers.org.

  4. Ona, kwa mfano, Saints: The Story of the Church of Jesus Christ in the Latter Days, vol. 1, The Standard of Truth, 1815–1846 (2018), 1:303–9.

  5. Joseph Smith, “Discourse, 28 April 1842,” 37, josephsmithpapers.org. Siku tatu baadae, Joseph Smith alihubiri mahubiri yaliyoelezea hekalu pale wazee wangepokea “funguo za ufalme” na “kupata endaumenti kutoka juu” (“Discourse, 1 May 1842, as Reported by Willard Richards,” 94, josephsmithpapers.org).

  6. Ona Charles C. Rich, diary, Apr. 12–16, 1836, katika Charles C. Rich Collection, Maktaba ya Historia ya Kanisa, Jiji la Salt Lake; tahajia na vituo vimesawazishwa.