Ujumbe wa Urais wa Eneo
Imani: Kichocheo cha Kupenda, Kushiriki na Kualika
Kila mmoja wetu ana fursa ya kupitia nyakati za imani kuu—nyakati ambazo, kwa ishara, inaweza kuhamisha milima. Bila kujali machimbuko yetu, imani ni kipawa kitakatifu kutoka kwa Baba yetu wa Mbinguni. Inatutia nguvu ya kusonga mbele, mara nyingi katika makoloni yasiyo salama, kwa ujasiri wa kushinda kila kikwazo.
Katika Kitabu cha Mormoni, Alma 32:21, Alma anafundisha kwamba “imani sio kuwa na ufahamu kamili wa vitu; kwa hivyo mkiwa na imani, mnatumainia vitu ambavyo havionekani, ambavyo ni vya kweli.” Maisha ya duniani yanaweza yakatia giza uelewa wetu wa uweza wa kiungu, lakini imani huwa kama kichocheo cha ukuaji wote na mabadiliko.
Nilipokuwa na miaka 19, familia yangu ilipoteza kila kitu. Maisha yalikuwa magumu sana kwa mama yangu, ndugu zangu na mimi mwenyewe. Yajayo yasiyojulikana yaliweka uzito mkubwa kwangu. Mara kwa mara tulikosa chakula cha kutosha, na ingawa mama yangu kwa ujasiri alificha mfadhaiko wake, ningeweza kuona kupitia kuigiza kwake. Kukata tamaa kulinikamata na niliangukia kwenye kukosa tumaini, nikiaminishwa kwamba maisha yangu kamwe hayatalinganishwa na chochote. Katika moja ya nyakati zangu za kukata tamaa, kwa makini nakumbuka sauti kwenye akili yangu ikiniuliza, “Je, hivi ndivyo maisha yako yatafika tamati? Hivi sivyo wewe ulivyo. Una nguvu ya kunyanyuka na kuangaza. Kuwa tu na imani kidogo.”
Kwa wakati ule, dada yangu mdogo alikuwa punde tu amejiunga na kanisa. Mara kwa mara alinialika nikahudhurie shughuli za Vijana waseja (YSA), lakini nilikataa—labda kutokana na kiburi, nikihisi kwamba ninapaswa kuonyesha njia kama kaka mkubwa. Hata hivyo, baada ya uamsho wangu mwenyewe, nilikubali mwaliko wake. Nilipowasili kwenye tukio la YSA, nilidhamiria nisionekane, nikakaa kimya nyuma. Lakini bado, msalimiaji mlangoni alinialika vizuri, na wengine walikuja kuzungumza nami kwa shauku ya dhati na wema. Walinikumbatia kama mmoja wao na kunialika kujiunga kwenye shughuli zao. kwa mshangao, nilikuwa nimezungukwa na vijana wa umri wangu ambao walikuwa wema na wenye shangwe kamili. Nilihisi kupendwa kikamilifu na kukubalika kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu.
Mzee Quentin L. Cook wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, katika Mkutano Mkuu wa kikao cha uongozi Oktoba 2024, alizungumza kuhusu nguvu ya kupenda, kushiriki na kualika. “Mara nyingi, kualika humaanisha kujumuisha familia zetu, rafiki na majirani katika kile ambacho tayari tunafanya. Kwa mfano, tunaweza kuwaalika:
-
Kujiunga pamoja nasi katika shughuli zetu za nyumbani.
-
Kujiunga nasi kwa ajili ya kuabudu na kujifunza injili.
-
Kuhudhuria matukio, kama vile kutoa baraka kwa mtoto au ubatizo.
-
Kushiriki katika shughuli za kata na jamii au huduma.
Mialiko ya mara kwa mara ya dada yangu kwenye shughuli za kanisa na upendo na kukubalika nilikopata kutoka kwa vijana ambao hawajaoa wala kuolewa vilibadilisha maisha yangu. Nilipokumbatia injili ya Yesu Kristo, imani yangu ilikua. Ingawa kesho yangu ilibakia kutojulikana, nilihisi tumaini na amani mpya. Nilibatizwa Aprili 1997, na kupitia ibada hiyo takatifu, nilikuja kuelewa kwamba sauti niliyoisikia wakati wa uamsho wangu hapo awali, ilikuwa ni Roho Mtakatifu. Nina shukrani kwa wenza wa daima wa Roho katika maisha yangu leo. Imani, hata katika kipimo chake kidogo, inaweza kuleta badiliko kuu. Mwokozi alifundisha katika Mathayo 17:20: “Mkiwa na imai kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.” Kupenda, kushiriki na kualika kulikotolewa kwangu na dada yangu na jamii ya YSA kuliniongoza kwa wamisionari na, hatimaye, kwenye maji ya ubatizo. Nilikabiliwa na mlima kwenye kugeuza maisha yangu na moyo wangu na hali zangu zilinibadilisha. Safari hii ilikuza ushuhuda wangu wa Yesu Kristo.
Leo, familia yangu (mke wangu na watoto) inafurahia baraka za injili, ikijumuisha fursa takatifu ya kuunganishwa hekaluni. Kutoka kwenye kukata tamaa hadi tumaini tukufu, tumemwagiwa baraka za Bwana. Ninashuhudia kwamba Yesu ni Kristo na kwamba tunaongozwa na nabii aliye hai leo. Katika jina la Yesu Kristo, amina.