2025
Kutana na Mshauri wa Pili Mpya wa Eneo la Kati la Afrika Mzee Christophe G. Giraud-Carrier na Dada Isabell Giraud-Carrier
Machi 2025


Kurasa za Karibu

Kutana na Mshauri wa Pili Mpya wa Eneo la Kati la Afrika Mzee Christophe G. Giraud-Carrier na Dada Isabell Giraud-Carrier

Mnamo Januari 2023 Christophe G. na Isabell Giraud-Carrier walialikwa kukutana na Rais Russell M. Nelson ofisini kwake.Wito ulitolewa kwa Christophe kuhudumu kama Sabini Mkuu mwenye Mamlaka katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kuanzia Aprili iliyofuata. Wito wa akina Giraud-Carrier kutoka kwa nabii wa huduma ya muda wote ya kanisa na ukubali wao ilikuwa mwendelezo kwa maisha yao ya imani, kujitoa, huduma na ushuhuda.

Christophe na Isabell wote wanatoka Ufaransa, watoto wa waongofu Kanisani ambao hadithi za uongofu wao zinafanana. Mnamo 1968, wakati akiishi Bordeaux Ufaransa, mchuuzi alikuja nyumbani kwa akina Mauclair—Dada Giraud-Carrier ni wa familia ya Mauclair. Mchuuzi wa zulia alisimulia hadithi yake na kuuza zulia kwa familia. Siku hiyo hiyo wamisionari wawili kutoka Kanisani waligonga hodi mlangoni. Wao pia walialikwa ndani na walisimulia hadithi yao. Matembezi ya aina mbili nyumbani kwa Mauclair yalisababisha ununuzi wa zulia jipya na uumini katika ufalme wa Baba wa Mbinguni duniani.

Christophe alizaliwa mnamo Januari 21, 1966, wa kwanza kati ya watoto saba waliozaliwa kwa Gerard na Annie Giraud-Carrier. Alipokuwa na miaka miwili, wazazi wake walikutana na wamisionari wawili kwenye mitaa ya Toulouse, Ufaransa na wakawapa wamisionari namba zao za simu. Wamisionari wale walipoteza namba ya simu na hawakupiga kabisa. Wamisionari waliofuatia walipata namba ya simu, wakawapigia, wakawatembelea, wakawafundisha na kuwabatiza akina Giraud-Carrier.

Wanandoa wa pande zote walijitoa kwa dhati kwenye injili ya Yesu Kristo wakiwafundisha watoto wao na kuhudumu popote walipoitwa. Walihudumu katika njia muhimu ikiwa ni pamoja na katika uongozi wa tawi na kata na katika miito ya uongozi wa wilaya na kigingi. Baba yake Isabel alikuwa tabibu katika vikosi vya ulinzi vya Ufaransa nafasi ambayo ilimpa fursa za kuhudumu katika nchi za nje. Kama matokeo, miaka kadhaa ya utoto ya Isabell aliishi huko Djibouti, New Caledonia na Algeria. Kanisa lilikuwa halijaanzishwa katika baadhi ya nchi hizo. Hivyo kuabudu na kuishi injili kulikuwa na kiini katika familia bila usaidizi wa taasisi ya kanisa. Sala ya familia na usomaji maandiko kama familia vilikuwa matendo yaliyozoeleka nyumbani, kama ilivyokuwa mikutano ya sakramenti ya kila wiki.

Mnamo mwishoni mwa miaka ya 1970 familia ya Mauclair ilirudi metropolitan Ufaransa, kwanza huko Auch (inatamkwa Osh) karibu na Toulouse. Mnamo 1978, walihamia kata ya Versailles, ambapo familia ya Mauclair na Giraud-Carrier walikuwa marafiki, na kijana Christophe akakutana na Isabelle kijana mdogo zaidi kwake.Urafiki huo wa utotoni ulikuwa hadi kwenye miadi, uchumba, kuvalishwa pete na ndoa. Baada ya muda fulani katika kata moja na kigingi kimoja, familia zilitengana, lakini mapenzi yaliyokuwa yakijengeka ya Christophe na Isabelle yaliendelea kukua kadiri walivyoendelea kuwasiliana kwa barua za mara kwa mara, simu za hapa na pale na muunganiko wa ana kwa ana katika robo nne za mwaka.

Mapema mnamo Julai ya mwaka 1986 Christophe alianza huduma ya umisionari katika Misioni ya Kanada Montreal. Alipokuwa Kanada, baba wa Isabelle alikuwa rais wa Isabelle wa wilaya ya Cholet Ufaransa. Baba yake alimwita kama mmisionari wa wilaya, akitimiza ahadi katika baraka yake ya patriaki. Isabelle alipangilia ratiba yake ya kazi ili kufanya kazi siku tatu kwa wiki na jioni zote akiwa na wamisionari. Wakati wa huduma yake, alikuwa sehemu muhimu ya kuwaleta takribani waongofu wapya 20 kanisani.

Wiki chache tu baada ya Christophe kurejea kutoka Misioni ya Kanada Montreak, wawili hao, ambao walikuwa wamekutana wakiwa wadogo miaka kumi kabla, walikuwa mume na mke mnamo Julai 16, 1988 huko Cholet Ufaransa. Siku tatu baadaye, ndani ya Hekalu la Bern, Switzerland, walikuwa na muunganiko wa milele. Christophe alikuwa na miaka 22.5 na Isabelle miaka 21.

Mnamo 1988, mwaka mmoja wa huduma ya jeshi ulihitajika kwa kila kijana wa kiume wa Ufaransa. Muda mfupi baada ya ndoa yao, Christophe alichukuliwa kwenda jeshi la Ufaransa. Alipangiwa na kuhudumu kwenye Kikosi cha Anga kwa mwaka huo. Baada ya huduma yake jeshini, Christophe alihamishia miaka yake miwili ya chuo kwenda Chuo Kikuu cha Brigham Young Provo. Huko alipata shahada ya kwanza, shahada ya uzamili, na shahada ya uzamivu katika Sayansi ya Kompyuta.

Baada ya kupata shahada yake ya uzamivu, familia ilihamia Bristol, Uingereza ambapo Christophe alifanya kazi kama profesa wa sayansi ya kompyuta kwa miaka 6.5. Alipumzika kidogo kutoka kwenye mambo ya taaluma kwa kukubali nafasi ya umeneja kwenye kampuni ya ELCA Informatique huko Lausanne, Switzerland. Wakiwa Switzerland, walikuwa umbali wa masaa mawili tu kutoka kwa familia kwa mara ya kwanza ndani ya takribani miaka 13. Walifurahia kuishi Switzerland.

BYU mara kwa mara ilimuuliza Dk. Giraud-Carrier ikiwa angefikiria kukubali kuwa profesa kwenye kampasi ya Provo. Jibu daima lilikuwa “hapana.” Wakati wa safari ya kwenda Utah mnamo 2004 mwenyekiti wa idara ya Sayansi ya Kompyuta aliwauliza tena, “nini kitawafanya mje Utah?” Wote wawili Christophe na Isabelle walipata msukumo imara kwamba walipaswa kukubali uprofesa wa BYU. Walisema “ndiyo,” na kusonga mbele kwa ujasiri kwa mwelekeo ambao Bwana alikuwa akiufunua kwao.

Familia ya Giraud-Carrier wana watoto nane, wa kiume wanne na mabinti wanne. Watoto wao wanne walizaliwa baada ya kuwa wameondoka Provo. Leo, sita kati ya watoto wao wameoa na kuolewa. Na ni bibi na babu kwa wajukuu wazuri 18. Kote katika maisha yao, wamekubali na kukuza kila wito wa kanisa. Mzee Giraud-Carrier amehudumu kama askofu, rais wa kata na kigingi wa wavulana, rais wa misioni ya kigingi, mshauri mkuu, rais wa kigingi na rais wa misioni. Dada Giraud-Carrier amekuwa rais wa watoto wa kata, rais wa wasichana wa kata, na rais wa muungano wa usaidizi wa kata, mwalimu wa watoto, mmisionari wa wilaya, kiongozi wa misioni na dada mhudumiaji wa kipekee. Juu yake, Mzee Patrick Kearon amesema:“Ikiwa ningetakiwa kuvuka ukanda wa tambarare, ningetaka kuwa ndani ya mkokoteni wake.”