2025
Mbingu Zinafunguka
Machi 2025


Kurasa za Karibu

Mbingu Zinafunguka

“Mfuko wa Usaidizi wa Kifedha kwa Waendaji Hekaluni Wote ulianza mnamo 1992 kama njia ya kuzuru mara moja hekaluni kwa waumini wanaoishi nje ya Marekani na Kanada. Fedha yote imekusudiwa kwa waumini.” (Church Website)

Rais Thomas S. Monson aliwahimiza waumini katika Mkutano Mkuu wa Oktoba 2011 kuchangia kwenye mfuko huo. Waumini wanaotumia fedha hizo wanahitajika kuchangia kiasi wanachoweza. Rais Monson alisema kwamba, “wale wanaoelewa baraka za milele ambazo huja kutoka hekaluni wanaelewa kwamba hakuna dhabihu iliyo kuu, hakuna gharama iliyo nzito, hakuna mapambano yaliyo magumu ili kupokea baraka hizo.” Lakini kwa waumini wengi, dhabihu bado ni kitu kisichofikika” (As We Met Again, Liahona Aprili. 2011, 5).

Katika Eneo la Kati la Afrika, msisitizo wa hivi karibuni wa kutumia fedha hii umeleta matokeo ya waumini 1700 kuruhusiwa kwenda hekaluni katika kipindi cha miezi tisa ya 2024. Wale ambao wamefanya maagano ya hekaluni wanarejea katika kata zao na matawi yao na kuwahimiza waumini wengine wahudhurie. Ukuaji katika mambo ya kiroho unaathiri Eneo lote kwa kiwango chanya.

Wale walioweza kuhudhuria Hekaluni na kufanya maagano ya Hekaluni wanalizingatia hilo kama uzoefu wa kubadili maisha. Wanapata uzoefu wa baraka zilizozungumziwa na Rais Russell M. Nelson katika hotuba yake ya Mkutano Mkuu wa Aprili 2024. “Tunaahidiwa kwamba ndani ya hekalu tuweze ‘kupokea utimilifu wa Roho Mtakatifu.’ (Mafundisho na Maagano 109:15). Fikiria hilo linachomaanisha katika maana ya kuwa na mbingu kufunguka kwa kila mtafutaji wa dhati wa ukweli wa milele.” Rais Nelson anaendelea, “tumeelekezwa kwamba wale wote wanaoabudu ndani ya Hekalu watakuwa na nguvu ya Mungu na malaika ‘wanawalinda.’ (Mafundisho na Maagano 109:22). Ni kwa kiasi gani inaongeza ujasiri wako kujua kwamba, kama mwanamke au mwanamume mwenye endaumenti uliyekingwa na nguvu za Mungu, huitaji kukabiliana na maisha peke yako? Ni ujasiri gani hii inakupa kujua kwamba malaika hakika watakusaidia?” (Russell M. Nelson, Mkutano Mkuu, Aprili 2024).

Kwa sababu ya ukarimu wa waumini wa kanisa katika kuchangia Mfuko wa Usaidizi wa Kifedha kwa Waendaji Hekaluni, na tamanio la watakatifu wengi katika Eneo la Kati la Afrika la kupokea na kupata uzoefu wa baraka za hekalu, mamia kwa mamia ya maisha yamestawishwa kiroho milele.

Uzoefu Wetu wa Hekaluni

Na Screven Omondi, Kata ya Langata Nairobi

Kuabudu hekaluni ni kitu cha kale kama vile ilivyo milima. Wakati wowote Bwana alipokuwa na watu wa agano duniani, daima amewaamuru wainue mahekalu au sehemu takatifu za kimbilio sawasawa na Hema ya Kuabudia, ambapo anaweza kuja na kukaa, na kuwaelekeza watoto Wake katika njia za haki. Watafutaji wote wa dhati wa ukweli ambao wanaingia ndani ya maeneo haya matakatifu wakiwa na mioyo iliyovunjika na roho zilizopondeka wana fursa ya kufanya na kushika maagano matakatifu ambayo yana asili ya vyote viwili, kuokoa na kuunganisha.

Katika M&M 109:16 tunasoma kuhusu lengo maalumu la mahekalu. Kila hekalu linatumika kama “nyumba ya sala, nyumba ya kufunga, nyumba ya imani, nyumba ya kujifunza, nyumba ya utukufu, nyumba ya utaratibu, nyumba ya Mungu,” ikifanya mahekalu yawe kiini cha kuabudu kwetu.

Uunganishwaji Wetu

Mimi na mke wangu tulipata fursa ya kutembelea hekalu la Accra Ghana, tuna shukrani kwa mfuko wa usaidizi wa kifedha kwa waendaji hekaluni.Mchakato mzima ulifanyika katika subira na imani. Tulijifunza kusali kwa dhati na kumngojea Bwana kwa matamanio ya haki ya mioyo yetu. Sala zetu zilijibiwa mwezi mmoja uliopita, tulipopata taarifa kutoka Eneo la Kati la Afrika kwamba maombi yetu yameidhinishwa. Safari yetu kwa ndege ya kwenda na kurudi ilikuwa salama na isiyo na tafrani.

Mimi na mke wangu tuliunganishwa kwa muda na milele yote mnamo tarehe 29 ya Mei 2024. Ulikuwa uzoefu usiosahaulika - uzoefu ambao nitauthamini kwa maisha yangu yote. Baada ya kutumia siku nzima Hekaluni niliandika kwenye shajara yangu jioni ile “Nimehisi bubujiko kubwa la Roho leo wakati wa ibada ya kuunganishwa kwangu na Annet. Baraka zilizotamkwa juu yetu zapita ufahamu, na bado tuna shukrani kwamba Bwana mwema ametuona tunastahili kupokea baraka teule ambazo mbingu na dunia zinatoa. Maisha ya milele yanafikika.”

“Nina bahati kuwa na mke wangu kama mwenza wangu wa milele. Nisingeweza kuomba mwenza mwingine zaidi yake. Yeye ni msafiri mwenzangu katika njia inayoongoza kurudi nyumbani kwenye uwepo wa Baba yetu. Ninao ushahidi wa kushikika wa upendo na rehema ya Mungu, na nina shauku ya kujua ya baadaye.”

Roho ya Eliya

Kile kilichoongeza kwenye shangwe yetu ni fursa tuliyopata ya kufanya ubatizo wa uwakilishi kwa ajili ya babu yangu mzaa baba na bibi yangu mzaa mama. Kulikuwa na uwepo wa kipekee katika hewa pale mimi na mke wangu tulipobatizwa na kupokea endaumenti kwa niaba yao. Ninajua wanatabasamu kwa ajili yetu. Nilipata pia fursa moja ya kufanya ibada za mwanzo kwa ajili ya mababu wa waumini wawili wa kata yangu. Baadhi ya uzao wa waumini wa kata yetu waliishi miaka ya 1700. Ninahisi muunganiko maalumu kwa watu hawa japokuwa siwafahamu. Hii lazima iwe hisia ambayo Roho wa Eliya huleta kwa mioyo kuwageukia akina baba na akina mama—kwa mababu zetu. Nina kila ujasiri watu waliokufa ambao tuliwafanyia ibada za uwakilishi wamekusanyika salama kundini upande mwingine wa pazia. Ukusanyaji hakika ni kazi kubwa tunayoweza kuifanya sasa, na inatendeka pande zote mbili za pazia

Tanbihi

  1. Kutoka 25.

  2. Rais Russell M. Nelson, “Chaguzi kwa ajili ya Milele”, (Worldwide Devotional for Young Adults, May 1, 2022), ChurchofJesusChrist.org, Mei 14, 2022.

  3. Rais Russell M. Nelson, “Hope of Israel”, (Worldwide Youth Devotional, June 3, 2018), ChurchofJesusChrist.org Mei 14, 2022.