2025
Kwa Ajili ya Watoto Wakubwa
Machi 2025


“Kwa Ajili ya Watoto Wakubwa,” Rafiki, Machi 2025, 34–35.

Kwa Ajili ya Watoto Wakubwa

Maneno kutoka Kwako

Nina nukuu kutoka kwa Rais Susan H. Porter kwenye ukuta wangu. Inasema, “Maisha yetu ni matakatifu na yana maana na lengo. Kila mmoja wetu ni binti mpendwa [au mwana] mpendwa wa Mungu.”* Ninajua kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanamjali kila mmoja wetu.

Ava B., miaka 10, Arizona, Marekani

Siku moja rafiki alinialika kucheza mpira wa miguu. Nilikuwa nikivaa nguo zangu za michezo wakati nilipokumbuka ilikuwa Jumapili! Nilibadilisha na kuvaa nguo zangu za Jumapili na kwenda kanisani. Nilihisi furaha sana.

Adrián E., umri miaka 11, Beni Department, Bolivia

Mimi Hupeleleza Oliver

Oliver Cowdery alimsaidia Joseph Smith kwenye tafsiri ya Kitabu cha Mormoni. Walikutana huko Harmony, Pennsylvania, Marekani. Je, unaweza kumpata Oliver kwenye mtaa huu wenye shughuli nyingi?

Pongezi na Miunganiko

Tumia rangi mbili tofauti na kupeana zamu na rafiki kuchora mstari mlalo au wima kati ya nukta mbili. Unapochora mstari unaokamilisha kisanduku, paka rangi katika kisanduku chako. Endelea mpaka nukta zote ziwe zimeunganishwa!

Sasa hesabu miraba ambayo ina rangi yako ndani yake. Sema jambo moja zuri kuhusu mtu kwa kila mmoja unaohesabu!

Chemsha bongo ya Waanzilishi

Je, unaweza kubahatisha vitu hivi vilitumika kwa ajili gani katika nyakati za mwanzo za waanzilishi?

  1. kuponda karanga

  2. kutengeneza siagi

  3. kutengeneza sharubati ya maziwa

  4. kuvaa viatu

  5. kufanya kazi kwa kuni

  6. kushikilia simu

Ukurasa wa PDF ukiwa na nukuu na shughuli

Vielelezo na Brian Michael Weaver

  • “Masomo Kisimani,” Liahona, Mei 2022, 59–60.