2025
Margo na Paolo
Machi 2025


“Margo na Paolo,” Rafiki, Machi 2025, 33.

Margo na Paolo

Msaada kwa ajili ya Kazi ya Nyumbani

Margo anaweka kichwa chake kwenye dawati lake wakati Paolo anachungulia chumbani

UGH!

“Je, … uko SAWA?”

Margo anafunika uso wake kwa mikono yake huku Paolo akiingia ndani

La! Kazi hii ya nyumbani ni ngumu sana. Sitaweza kamwe kuipatia!

Pengine ninaweza kukusaidia.

Picha ya karibu sana ya Margo mikono yake ikiwa juu ya uso wake

Hakuna haja. Mimi si mwerevu kama wewe.

Paolo anasimama karibu na dawati na kutabasamu kwa kumtia moyo Margo

Unaweza kufanya hili. Unahitaji tu msaada kidogo—na hiyo ni SAWA! Nilipata msaada kutoka kwa Baba.

Paolo anakaa kando ya Margo kwenye dawati akitabasamu

Nilimuomba pia Baba wa Mbinguni anisaidie nielewe. Je, unataka kusali?

Wazo zuri.

Margo na Paolo wakisali na kisha kujifunza pamoja

Baadaye …

Margo akiwa ameshikilia karatasi yenye nyota ya dhahabu juu yake na kugonganisha kiganja chake na cha Paolo

Unaona? Nilijua ungepatia.

Asante kwa kunisaidia!

Ukurasa wa PDF

Vielelezo na Katie McDee