2025
Anika Jasiri
Machi 2025


“Anika Jasiri,” Rafiki, Machi 2025, 44–45.

Anika Jasiri

Hadithi ya kweli kutoka Marekani.

Mwanamke akiwa amepiga magoti mbele ya msichana mdogo

“Je, uko tayari?” Mama aliuliza.

Anika alikubali kwa kichwa na kukumbatia mdoli wake. Alikuwa amekuja naye kanisani. Alitumaini angemsaidia ili ahisi kuwa jasiri.

Anika alikuwa na sehemu ya kusema katika programu ya Watoto leo. Lakini alikuwa mpya kwenye nchi hii. Hakuzungumza Kiingereza kingi. Alikuwa anaenda kusema kwa Kihispania. Je, kila mtu angeelewa?

Mwanamke akimkumbatia msichana mdogo

Mami alimpa kumbatio. “Najua una wasi wasi. Lakini kumbuka, Roho Mtakatifu atakuwa pamoja nawe! Hauko peke yako.”

Hiyo ilimfanya Anika kuhisi vizuri kidogo. Alitoa tabasamu kwa mdoli wake. Kisha kutakuwa na watatu kati yetu, aliwaza. Mimi, mdoli wangu, na Roho Mtakatifu!

Watoto wakiwa wamekaa kwenye jukwaa

Katika programu ya Watoto, darasa la Anika lilizungumza kuhusu kile walichojifunza mwaka huo. Walienda kwenye jukwaa mmoja baada ya mwingine. Punde iliwadia zamu ya Anika.

Alikumbatia mdoli wake. Angeweza kuwa jasiri!

Msichana mdogo akiwa amesimama kwenye mimbari

“Familia yangu inajifunza maandiko pamoja na Njoo, Unifuate kila usiku,” Anika alisema kwa Kihispania. Alivuta pumzi kwa nguvu. “Tulijifunza jinsi Joseph Smith alivyowasamehe wale waliomumiza. Ninaweza kuwasamehe wengine pia. Katika Jina la Yesu Kristo, amina.”

Anika alirudi kwenye kiti chake. Mwalimu wake alitabasamu kwake na kwa mdoli wake. “Kazi nzuri,” alinong’ona. “Ninyi nyote mlikuwa jasiri sana!”

Anika alihisi vizuri moyoni mwake. Alikuwa amekuwa jasiri! Na alijua Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye.

Mwalimu wa Watoto akizungumza na msichana mdogo
PDF ya hadithi

Vielelezo na Katie Rewse