“Kumfuata Yesu huko Madagaska,” Rafiki, Machi 2025, 10–11.
Kumfuata Yesu huko Madagaska
Kutana na Lauren
Lauren anamfuata Yesu Kristo kwa kuwa mfano mzuri na kutii amri za Mungu. Wakati mmoja alikuwa na wakati mgumu katika darasa lake la masomo ya kijamii. Japokuwa ilikuwa vigumu kujifunza, alisema, “Nilimwomba Mungu, na Yeye akanipa ufahamu wa kuelewa.”
Kuwasaidia wengine kunamfurahisha. Anasema, “Ninahisi shangwe kwa sababu ningeweza kufuata mfano wa Kristo wakati Yeye alipowasaidia wengine.”
Kuhusu Lauren
Umri: miaka 9
Kutoka: Mkoa wa Sofia, Madagaska
Lugha: Kimalagasi na Kifaransa
Lengo: Kuwa rubani kwa sababu anapenda kuruka kwa ndege
Shughuli za muda wa ziada: Kucheza soka, kucheza michezo na familia, na kusoma vitabu
Familia: Lauren, Baba, na kaka wanne
Mambo Ayapendayo
Hadithi ya Maandiko: Andiko pendwa la Lauren kuhusu Yesu Kristo ni hadithi ya kuzaliwa Kwake ( ona Mathayo 1:18–25; 2; Luka 1:26–38; 2:1–20) kwa sababu inatuambia kwamba Mwokozi wetu alizaliwa ili kutuokoa.
Tunda na mboga: Tufaa na boga
Chakula: Piza
Rangi: Waridi
Wimbo wa Watoto: “When I Am Baptized” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 103)