“Kufukuza Vivuli kwa Kuimba,” Rafiki, Machi 2025, 16–17.
Kufukuza Vivuli kwa Kuimba
Ghafla maneno ya wimbo wake pendwa wa Darasa la Watoto yaliingia kichwani.
Hadithi ya kweli kutoka Mexico.
“Muda wa kulala,” Mamá alisema kwa tabasamu.
Logan alikwenda chumbani kwake. Alisema sala zake na kutambaa kitandani. Kisha Mamá akamsomea hadithi. Taratibu alifumba macho yake. Punde alisinzia.
Lakini Logan alikuwa na ndoto ya kutisha. Alikuwa peke yake katika mahali penye giza. Aliona jinamizi kubwa, lenye miiba lililo na meno makubwa. Lilimuungurumia. Kisha likaanza kukimbia kumuelekea!
Logan alijaribu kukimbia. Lakini aliteleza na kuanguka! Jinamizi lilikaribia zaidi sana na kuwa kubwa zaidi hadi—
Logan alipoamka na kukaa kitandani. Alifuta machozi kutoka machoni mwake na kuona bado kulikuwa na giza nje.
Alitaka kuzungumza na wazazi wake kuhusu ndoto ile. Lakini hakutaka kuondoka kitandani mwake. Giza lilimfanya ahisi kama jinamizi lilikuwa limejificha mahali fulani. Kila kivuli kilionekana cha kuogofya. Mbwa aliyebweka huko nje alisikika kama jinamizi likinguruma.
Logan alijifunika shuka hadi kwenye pua yake. Alikuwa na uoga sana kufanya chochote.
Alitaka kurudi kulala. Lakini kila mara alipofumba macho yake, aliona uso wenye hasira wa jinamizi na meno yenye ncha kali. Hakuweza kuacha kuangalia vivuli vya kutisha.
Kisha akaona picha mezani kando ya kitanda chake. Ilikuwa ni picha yake, kaka zake wawili, Papá, na Mamá nje ya hekalu huko Monterrey, Mexico. Walionekana kuwa na furaha sana.
Ghafla, maneno ya wimbo wake pendwa wa Msingi yaliingia kichwani mwake. “Ninapenda kuliona hekalu,” Logan alianza kuimba kwa utulivu. “Nitaenda huko siku moja. Kumhisi Roho Mtakatifu, kusikiliza na kusali.”*
Wakati akiimba, Logan alifikiria kuhusu siku ile hekaluni pamoja na familia yake. Alikuwa amehisi amani sana. Kwa sababu ya hekalu, angeweza kuwa pamoja na familia yake milele.
Logan hakuweza kumsikia mbwa akibweka juu ya sauti yake. Alifumba macho yake na akaendelea kuimba. “Kama mtoto wa Mungu, nimejifunza ukweli huu: Familia ni ya milele.” Alihisi amani moyoni mwake ambayo ilimfanya atabasamu. Alijua hapakuwa na jinamizi.
Chumba kilikuwa kimejaa giza na cha kuogofya. Lakini sasa kilikuwa mahali patulivu, salama. Logan aliegemea tena kwenye mto wake na kulala kwa amani.
Alipoamka, kulikuwa na jua angavu nje. Aliamka na kutazama mwangaza wa jua ukiakisi picha yake ya hekalu. Aliimba wimbo wake pendwa kwa kutoa tu sauti mdomoni alipokuwa akijiandaa kwa ajili ya kwenda kanisani.
Akiwa njiani kwenda kanisani, aliiambia familia yake kuhusu jinamizi lake na wimbo aliouimba. Alisikiliza hotuba na kuimba nyimbo kanisani. Kisha ukafika wakati wa kwenda Darasa la Watoto.
Logan alipenda kusikiliza kinanda. Na sasa alijua kwamba baadhi ya nyimbo zina nguvu za kutosha kufanya hata majimamizi ya kutisha kuondoka.
“Karibuni katika wakati wa kuimba,” alisema kiongozi wa Darasa la Watoto. “Ni wimbo gani tunapaswa kuuimba kwanza?”
“Najua!” alisema Logan, akinyanyua mkono wake juu hewani. “Acha tuimbe ‘Napenda Kuliona Hekalu.”
Vielelezo na Carolina Farías