“Ukuhani Umerejeshwa,” Rafiki, Machi 2025, 26–28.
Hadithi za Maandiko
Ukuhani Umerejeshwa
Unaweza kusoma hadithi hii katika Joseph Smith—Historia ya 1:66–73 na Mafundisho na Maagano 27:12.
Baada ya Joseph Smith kupokea mabamba ya dhahabu, alianza kuyatafsiri. Oliver Cowdery aliandika kile alichokisema. Walipokuwa wakifanya kazi, walijifunza kwamba Yesu Kristo alitaka kila mtu abatizwe.
Joseph na Oliver walijiuliza ni nani alikuwa na nguvu za Mungu za kubatiza watu. Walienda msituni kusali na kumuuliza Mungu.
Walipokuwa wakisali, malaika alitokea. Alisema alikuwa Yohana Mbatizaji, aliyembatiza Yesu Kristo zamani za kale. Aliwapa Joseph na Oliver Ukuhani wa Haruni ili waweze kuwabatiza wengine. Ukuhani ni nguvu ya Mungu. Unatumika kuwabariki watoto wa Mungu.
Yohana Mbatizaji aliwaambia Joseph na Oliver wabatizwe. Walikwenda kwenye mto na kubatizana. Walipotoka majini, walijazwa na Roho Mtakatifu. Walikuwa na furaha sana.
Baadaye, malaika wengine walikuja. Watatu kati ya Mitume wa Yesu Kristo—Petro, Yakobo, na Yohana—waliwapa Joseph na Oliver Ukuhani wa Melkizedeki. Sasa Joseph na Oliver wangeweza kutoa kipawa cha Roho Mtakatifu kwa wengine.