“Shughuli za Njoo, Unifuate,” Rafiki, Machi 2025, 22–23.
Shughuli za Njoo, Unifuate
Februari 24–Machi 2: Mafundisho na Maagano 18
Picha Binafsi
“Thamani ya nafsi ni kubwa mbele za Mungu” (Mafundisho na Maagano 18:10). Hiyo inamaanisha kwamba kila mtu ni muhimu kwa Baba wa Mbinguni, ikijumuisha wewe! Chora picha yako mwenyewe. Jaribu kuipamba kwa vifaa tofauti vya sanaa! Juu yake, andika “Mungu Ananipenda.”
Machi 3–9: Mafundisho na Maagano 19
Masikio ya Kusikiliza
Yesu Kristo anatuomba tumsikilize Yeye ( ona Mafundisho na Maagano 19:23). Wasikilizaji wazuri hukumbuka kile walichosikia. Ketini katika mduara Mtu mmoja ananong’ona neno la injili. Mtu anayefuata analirudia na kuongeza jipya. Nendeni kwa kuzunguka duara mpaka kila mmoja ameongeza neno la kukumbuka!
Machi 10–16: Mafundisho na Maagano 20–22
Mnara wa Urejesho
Yesu Kristo alirejesha Kanisa Lake leo jinsi lilivyokuwa wakati alipokuwa duniani (ona Mafundisho na Maagano 20). Wekea alama vikombe vya plastiki kwa baraka tulizonazo kama sehemu ya Kanisa la Yesu Kristo, kama vile ukuhani, ubatizo, manabii. Kisha pangeni vikombe vyenu kuwa mnara mrefu!
Machi 17–23: Mafundisho na Maagano 23–26
Nyimbo za Moyoni
Baba wa Mbinguni anapenda tunapoimba kutoka mioyoni mwetu (ona Mafundisho na Maagano 25:12). Chagua baadhi ya nyimbo za Darasa la Watoto za kuimba pamoja. Buni vitendo vya kuendana na maneno ya wimbo.
Machi 24–30: Mafundisho na Maagano 27–28
Nabii Anasema
Nabii hupokea ufunuo kutoka kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kwa ajili ya Kanisa (ona Mafundisho na Maagano 28:7). Chapisha au chora picha ya nabii. Juu yake, andika “Nabii anasema …” Andika au chora mambo ambayo nabii wetu ametufundisha.
Picha na Christina Smith