2025
Kutafuta Tumbili
Machi 2025


“Kutafuta Tumbili,” Rafiki, Machi 2025, 4–5.

Kutafuta Tumbili

“Ni kama vile ninavyoweza kumsikia Roho Mtakatifu ninaposikiliza.”

Hadithi ya kweli kutoka Costa Rica.

Mvulana aliyevaa miwani ya jua akiwa amekasirika wakati msichana na mvulana nyuma yake wakitabasamu na kuonyesha kitu nje ya fremu.

“Whoa!” Ethan alisema. “Je, umemuona huyo?”

“Ndio, angalia mkia wake mdogo mzuri!” alisema Lily.

Boston alitazama juu, lakini aliona tu vivuli.

“Tayari tumeshaona tumbili watatu leo!” Ethan alisema.

Lakini Boston hakuwa ameona yeyote! Familia yake ilikuwa ikitembelea msitu wa mvua kuona tumbili mwitu. Lakini tumbili walikuwa mbali sana kwa Boston kuwaona.

Boston alikuwa kipofu. Angeweza tu kuona vitu vilivyo karibu naye. Kwa kawaida, hakujali kuwa kipofu. Angeweza bado kufanya mambo mengi mazuri. Angeweza kusoma Braille kwa vidole vyake na kutembea na fimbo yake gizani. Na angeweza kuwapata watu kwa kusikiliza sauti zao.

Lakini wakati mwingine, Boston hakupenda kuwa kipofu. Kama leo.

Boston aliketi ardhini na kuvuta pumzi. Sio haki! aliwaza.

Dakika chache baadaye alipata wazo. Baba wa Mbinguni, tafadhali msaidie tumbili aje karibu vya kutosha kwa mimi kumwona, Boston alisali akilini mwake.

Boston bado hakuweza kuona tumbili yeyote. Kisha akasikia kelele kutoka mbali sana.

Mvulana aliyevalia miwani ya jua akitabasamu wakati akiweka kiganja nyuma ya sikio ili kupata usikivu mzuri

“Umesikia hilo? Boston aliuliza. “Nadhani ilikuwa ni tumbili.”

“Sikusikia chochote,” Ethan alisema.

“Wala mimi sikusikia,” Baba alisema. “Una masikio mazuri!”

Boston alisikia tumbili akikimbia kupita vichaka kando ya njia. Boston alionyesha kuelekea kwenye sauti ile. “Hapo juu!”

Kisha akasikia mwingine, na mwingine. Wakati mwingine familia yake iliweza kuona tumbili wakati alipowaonyesha. Lakini hakuna hata tumbili aliyekaribia vya kutosha kwake kuweza kuona.

Mvulana aliyevalia miwani ya jua akiwa na kiputo cha usemi kikionyesha mawimbi ya sauti

Punde ikawa wakati wa kwenda nyumbani.

“Nasikitika hukuona tumbili yeyote,” Mama alisema walipokuwa wakitembea kuelekea kwenye gari.

Boston alipandisha mabega. “Ni SAWA. Nilitaka kuona mmoja, lakini badala yake nilipata kuwasikia wengi.” Kisha akawaza kuhusu sala yake. “Ni kama inanikumbusha mimi juu ya Roho Mtakatifu.”

“Unamaanisha nini?” Mama aliuliza.

“Niliposimama kusikiliza, niligundua wote walikuwa karibu nami. Niliweza kuwasikia japokuwa sikuweza kuwaona. Ni kama vile ninavyoweza kumsikia Roho Mtakatifu ninaposikiliza.”

“Hilo ni somo zuri sana,” Mama alisema.

Boston alisikia kitu fulani katika vichaka karibu naye. Kisha kitu fulani kilikimbia kwenye njia—mbele yake kabisa! Kilikuwa na nywele nyekundu na mkia mrefu. Kilisimama na kumwangalia vizuri. Kisha kikakimbia tena kwenye miti.

Tumbili! Hatimaye alipata kumwona mmoja!

Boston alitabasamu. Kuwa kipofu ilikuwa vigumu wakati mwingine. Lakini leo, ilimsaidia kujifunza kuhusu Roho Mtakatifu. Na hiyo ilikuwa nzuri sana.

tumbili wa rangi ya machungwa
PDF ya hadithi

Vielelezo na Alyssa Gonzalez