“Amani kutoka Hekaluni,” Rafiki, Machi. 2025, 2–3.
Kutoka Urais wa Kwanza
Amani kutoka Hekaluni
Imetoholewa kutoka “Yote Yatakuwa Sawa Kwa Sababu ya Maagano ya Hekaluni,” Liahona, Mei 2024, 24–27.
Miaka kadhaa iliyopita, mimi na mke wangu tuliendesha gari kwenda kutembelea Hekalu la Idaho Falls Idaho. Vijana wetu wanne walibaki nyumbani na mlezi wa muda.
Tulipokuwa tayari kwenda nyumbani, mmoja wa wafanyakazi wa hekalu alituambia kwamba Bwawa la Teton mashariki mwa Idaho lilikuwa limebomoka! Sehemu kubwa ya jiji letu ilikuwa imefurika maji.
Mimi na mke wangu tulipiga magoti na kuomba kwa Baba wa Mbinguni kwa ajili ya usalama wa watoto wetu na maelfu ya watu walioathirika kwa mafuriko. Maneno haya yalikuja wazi moyoni mwangu na akilini: “Matokeo yoyote yatakayotokea, yote yatakuwa sawa kwa sababu ya hekalu.” Tulikuwa na shukrani baadaye kujifunza kwamba wavulana wetu walikuwa salama.
Hakuna chochote kilicho muhimu kuliko kuyaheshimu maagano utakayoyafanya siku moja hekaluni. Bila kujali chochote kile, yote yatakuwa sawa kwa sababu ya maagano ya hekaluni.
Mzingile wa Hekalu
Hekalu linaweza kutuletea amani katika nyakati ngumu. Fuata mzingile hadi juu ya Hekalu la Idaho Falls Idaho!
Vielelezo na Alyssa Tallent