“Maneno Yangu ya Injili,” Rafiki, Machi 2025, 6.
Maneno Yangu ya Injili
Tafuta maneno haya na virai katika toleo hili la Rafiki!
Ibada
Ibada ni tendo tukufu, au takatifu, linalofanywa kwa mamlaka ya ukuhani katika jina la Yesu Kristo. Baadhi ya mifano ni sakramenti, ubatizo na uthibitisho.
Ondoleo la Dhambi
Tunapotubu na kupokea ondoleo la dhambi, tunasamehewa kwa chaguzi mbaya tulizozifanya. Hili linawezekana kwa sababu ya Yesu Kristo.
Mpole
Kuwa mpole ni kuwa mnyenyekevu, mtulivu, kuwa radhi na mtiifu. Yesu Kristo aliweka mfano wa hili wakati alipokuwa duniani.
Watakatifu
Katika Agano Jipya, watakatifu walikuwa wale wote waliochagua kubatizwa na kujiunga na Kanisa la Yesu Kristo (ona Matendo ya Mitume 9:13). Tunatumia neno hilo hilo kwa wale wanaochagua kubatizwa katika Kanisa Lake leo. Mtakatifu ni mtu anayemfuata Yesu Kristo.
Vielelezo na Madison Baker