“Kadi za Mahekalu,” Rafiki, Machi 2025, 12.
Kadi za Mahekalu
Hekalu la Salt Lake
-
Waanzilishi walijenga hekalu hili kwa matale kutoka korongo kuu lililo karibu. Baadhi ya mawe yalikuwa na uzito wa paundi 5,600 (kilo 2,540)!
-
Lilichukua miaka 40 kukamilika.
-
Wasanii watano waliitwa kwenye misheni kusoma sanaa nchini Ufaransa. Baadaye, walichora picha za ukutani ndani ya hekalu.
Hekalu la Cape Town Afrika Kusini
-
Hili litakuwa hekalu la tatu huko Afrika Kusini.
-
Wamisionari walikuja katika eneo mnamo 1852. Sasa Afrika Kusini ina takribani ya waumini wa Kanisa 70,000.
-
Hekalu lililo karibu linakaribia maili 795 (kilomita 1,280) huko Durban.
Hekalu la Lima Peru
-
Hekalu hili lina minara sita. Ule ulio mrefu zaidi una futi 112 (mita 34).
-
Baadhi ya Watakatifu walisafiri kwa basi kwa saa 26 kuhudhuria uwekaji wakfu.
-
Wakati Hekalu la Lima Peru Los Olivos lilipowekwa wakfu, Lima ukawa mji wa kwanza nje ya Marekani kuwa na mahekalu mawili.
Vielelezo na Rachel Erickson