2025
Pata Kuyajua Mabamba ya Dhahabu!
Machi 2025


“Pata Kuyajua Mabamba ya Dhahabu!,” Rafiki, Machi 2025, 24–25.

Pata Kuyajua Mabamba ya Dhahabu!

Fuata mfululizo wa matukio ili kuona jinsi tulivyopokea Kitabu cha Mormoni.

  • ~421 BK

  • Moroni, nabii wa Kitabu cha Mormoni alifunga mabamba ya dhahabu. Mabamba haya yalifundisha kuhusu Yesu Kristo. Pia yalielezea historia ya watu wa Moroni.

  • 1823

  • Kama malaika, Moroni alimtembelea Joseph Smith. Moroni alimwambia mabamba ya dhahabu yalikuwa yamezikwa karibu na Mlima Kumora.

  • 1827

  • Baada ya Joseph kujiandaa kwa miaka minne, Bwana alimwamini aende na mabamba hayo nyumbani.

  • 1828

  • Joseph alitafsiri mabamba kwa kumsikiliza kwa makini Roho Mtakatifu. Pia alitumia vifaa maalumu kutoka kwa Mungu. Alitumia jiwe lililoitwa jiwe la mwonaji na vifaa vinavyoitwa vikalimani au Urimu na Thumimu ambavyo vilikuwa vimezikwa pamoja na mabamba.

  • 1829

  • Baba wa Mbinguni alimsaidia Joseph kuelewa kile ambacho mabamba yalisema. Oliver Cowdery alisaidia kuandika kile Joseph alichotafsiri.

  • Angalau watu kumi na wawili waliyaona yale mabamba ya dhahabu. Mmoja wao alikuwa ni Mary Whitmer. Unaweza kusoma ushuhuda wa mashahidi wengine kwenye ukurasa wa mbele wa Kitabu cha Mormoni. Hakuna kati ya watu hawa aliyewahi kukana walichokiona na kukipitia.

  • 1830

  • Nakala ya kwanza iliyotafsiriwa ya Kitabu cha Mormoni kwa Kiingereza ilichapishwa Palmyra, New York, Marekani.

  • Leo

  • Kitabu cha Mormoni sasa kinasomwa kote ulimwenguni! Kimetafsiriwa katika lugha 115. Wamisionari wanashiriki Kitabu cha Mormoni na kila mtu wanayeweza kushiriki naye.

Mfululizo wa matukio ulio na vielelezo vya Joseph Smith na mabamba ya dhahabu

Vielelezo na Alyssa Petersen