Kurasa za Karibu
Imani na Shangwe huku Akivuka Malengo ni Sifa Bainifu za Rais Mpya wa Eneo la Kati la Afrika
Mzee Thierry K. Mutombo, Rais Mpya wa Eneo la Kati la Afrika na Mkewe, Dada Nathalie Mutombo kwa Uaminifu Wamefanya Kazi Kupitia Mateso na Kuishi Maisha kwa Shangwe.
Yeyote ambaye amekutana na Mzee Thierry K. Mutombo mara moja, mara mbili, au mara kumi atakuwa amepata uzoefu wa “habari” kwa sauti shupavu, tabasamu la bashasha na kumbatio. kwa wanaume, daima kumekuwa na kumbatio. salamu zake zinaakisi maisha ya shangwe. Mzee Mutombo, na mkewe Nathalie, wamepitia uzoefu wa magumu ya kuvunja moyo. shangwe yao ina msingi katika shuhuda zao imara za Injili ya Yesu Kristo na imani katika mpango mkuu wa Mungu wa furaha kwa ajili ya watoto Wake.
Mnamo tarehe 1 Agosti, 2024, Mzee Mutombo alikuwa Rais wa Eneo la Kati la Afrika la Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Mzee Mutombo, sambamba na washauri wake, Mzee Paul B. Pieper na Christophe G. Giraud-Carrier, watakuwa wakilisimamia kanisa katika nchi 11 za Afrika ya Kati ambapo Kanisa limeidhinishwa. Eneo linasambaa kuanzia Bahari ya Hindi na Kenya na Tanzania upande wa mashariki kuelekea Bahari ya Atlantic na Cameroon, na Jamhuri ya Kongo upande wa Magharibi. Kuna waumini 192,000 katika Eneo. Uumini katika Kanisa umekua kwa 54% tangu kuanzishwa kwa Eneola Kati la Afrika mnamo 2020.
Mzee Mutombo pamoja na familia yake walijiunga na kanisa huko Kinshasa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakati alipokuwa na miaka kumi. Dada Mutombo alijiunga na kanisa miaka kadhaa baada yake wakati alipokuwa na miaka tisa. Dada yake aitwaye Hope alikuwa amekutana na wamisionari. Kwa baraka za wazazi wao, Nathalie na Hope walibatizwa. Miaka mitano baadaye mama yao alifariki. Miaka miwili baada ya hilo, baba yao alifariki.
Katika umri wa miaka 19, Mzee Mutombo aliitwa kutumikia misioni katika Misheni ya Cote D’Ivoire Abidjan. Askofu wake alimhimiza asome Kitabu cha Mormoni mwanzo hadi mwisho kabla ya kuanza misioni yake. Kwa miezi mitatu alikwenda kila siku kwenye jengo la kata yake ili kusoma, kutafakari na kusali kuhusu Kitabu cha Mormoni. Uzoefu huu wa usomaji wa kila siku ulileta matokeo ya yeye kupeleka katika misioni yake ushuhuda imara juu ya kitabu. Yeye amesema “nyenzo kuu ambayo tunayo ya kuwaleta watu katika nuru ya injili na kuikusanya Israeli iliyotawanyika ni Kitabu cha Mormoni.”
Misioni yake ilikuwa na athari kubwa kwenye maisha yake. Kifaransa ndiyo lugha kuu ya DRC na Cote D’Ivoire. Thierry alikuwa na wenzake kadha wa kadha waliozungumza Kiingereza. Rais wake wa misioni alimshauri atenge muda kila siku wa kujifunza Kiingereza kutoka kwa wenzake na Mzee Mutombo kwa utiifu aliongeza kujifunza lugha ya Kiingereza kwenye kujifunza kwake injili na kufundisha injili. Weledi wake wa lugha ya Kiingereza na Kifaransa umewabariki wengi.
Nathalie pia alihudumu misioni. Aliitwa kwa mara ya kwanza kuhudumu Nigeria. Kuchelewa kupokea viza kwa ajili ya kwenda Nigeria kulidumu kwa muda mrefu wa misioni yake hivyo alipangiwa upya kuhudumu katika nchi yake. Hili lingethibitika kuwa bahati nasibu kwani ilikuwa wakati alipokuwa akihudumu katika kata ya Kinshasa ndipo alipofahamiana na wazazi wa Mzee Mutombo. Mama yake Mutombo alimwambia kijana wake kuhusu Dada Nathalie Sinda. “Kuna dada mmisionari katika kata yetu, na ni wa kustaajabisha sana. Ikiwa siku moja utamuoa yule dada mmisionari, utakuwa mwanamume mwenye furaha zaidi.”
Miezi kadhaa baada ya mazungumzo na mama yake, Mzee Mutombo aliwatembelea baadhi ya marafiki. Nathalie Sinda, ambaye alikuwa amerejea nyumbani kutoka kwenye misioni yake siku moja nyuma, alikuwa kwenye nyumba ile. Akikumbuka pendekezo la mama yake, aliamua kumuomba Dada Nathalie waende kwenye miadi. Mwaka mmoja baadaye, walioana.
DRC ni nchi ya pili masikini ulimwenguni. Mnamo 2002, wastani wa pato la mtu kwa mwaka lilikuwa chini ya $100 (Dola za Kimarekani). Mnamo tarehe 29 Novemba, 2002, walioana katika sherehe ya kiserikali. Penzi lao lilikuwa tele, pesa haikuwepo. Baada ya kufunga ndoa, wanandoa wapya walikwenda kwenye jengo la kata yao ambapo waumini walikuwa wametengeneza donati na juisi na kuwaalika marafiki kuwapongeza wanandoa vijana. Takribani miaka miwili baadaye, mnamo tarehe 19 Novemba, 2004, waliunganishwa kwa muda na milele yote ndani ya Hekalu la Johannesburg, Afrika Kusini.
Bidii na uaminifu, huduma yenye juhudi daima vimekuwa sehemu ya maisha ya pamoja ya Mzee na Dada Mutombo. Kuvunjika moyo na mateso pia vimekuwa sehemu ya maisha. Wanne kati ya watoto sita wa akina Mutombo walifariki wakiwa wachanga. Mdogo alifariki akiwa na wiki moja, na mkubwa katika vifo hivi vya ghafla katika umri wa uchanga, alifariki akiwa na miezi 9. Katika hali ya kuvunjika moyo ya kupoteza wanne kati ya watoto sita, imani ya Mzee na Dada Mutombo katika Mungu na upendo kati yao havikuyumba. Leo hii, wana watoto hai sita, Jason, Blessing, Ariel, Marvel, Harvest, na Ruby. Ruby, mtoto wao wa 10 na binti wa 3, alizaliwa wakati akina Mutombo wakiongoza misioni ya Maryland Baltimore.
Mnamo 2018, katika umri wa miaka 42, Mzee na Dada Mutombo walianza huduma kama viongozi wa Misioni ya Maryland Baltimore. Juhudi ya Mzee Mutombo katika kujifunza Kiingereza wakati akihudumu kama mmisionari sasa ilikuwa ulazima katika jukumu lake jipya. Katika tukio moja, katika huruma nyororo na kwa wakati, Mzee Mutombo alipata ndoto dhahiri ambapo aliona nyayo za Yesu. Alizikaribia nyayo hizo na kuweka mguu wayo wake ndani ya moja ya nyayo hizo. Ulitosha kikamilifu. Alitambua, kwamba kama mtumishi wa Mungu, alikuwa akifuata nyayo za Yesu.
Mnamo Desemba ya 2019, wakati akihudumu huko Baltimore, walialikwa kukutana na Rais wa Kanisa Russel M. Nelson. Mkutano ulikuwa kwa njia ya mtandao. Nabii alimuuliza Mzee Mutombo mwenye miaka 43 juu ya lipi lilikuwa jambo muhimu walilokuwa wamejifunza kwenye misioni yao. Rais Mutombo alijibu, “kujaribu kufuata nyayo za Mwokozi kila siku.” Rais Nelson kisha akatoa wito kwa Mzee Mutombo kuhudumu kama Sabini Mkuu mwenye Mamlaka. Kwa miaka 27 ambayo ingefuata, atajitolea maisha yake katika kazi ya Mwokozi. Mnamo Jumamosi mchana, tarehe 4 Aprili, 2020,wakati wakitazama mkutano mkuu kama familia huko Baltimore, Maryland, watoto sita wa Mutombo walifahamu kuhusu jukumu jipya la baba yao. Kutembea katika nyayo za Mwokozi kungeendelea kwa miaka mingi.
Mnamo Agosti ya 2020, Mzee Thierry K. Mutombo aliungana na Rais wa Eneo Joseph Sitati na Mshauri wa Kwanza Matthew Carpenter kama Urais wa kwanza wa Eneo katika Eneo jipya la Afrika ya Kati. Hivi leo, kama Rais wa Eneo, Mzee Mutombo huleta maisha ya imani, huduma ya kujitolea, ya shangwe katikati ya changamoto, na ya upendo kwenye jukumu lake jipya.