2025
Je, Wito Wangu wa Misheni Ulikuwa Kosa?
Januari 2025


“Je, Wito Wangu wa Misheni Ulikuwa Kosa?” Liahona, Januari 2025.

Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Je, Wito Wangu wa Misheni Ulikuwa Kosa?

Nilipokuwa mbali sana na nyumbani, Bwana alinisaidia kugundua jinsi ya kushiriki upendo Wake.

mmisionari kwenye baiskeli

Miaka miwili katika shahada yangu ya hisabati na fedha, nilikuwa na msukumo mkubwa wa kwenda misheni. Nilichagua kutumikia, ingawa ningeweza kuacha baadhi ya mahitaji ya chuo ambayo ilibidi yachukuliwe mfululizo.

Muda mfupi baadaye, niliposoma wito wangu wa misheni kwenda Misheni ya Utah Salt Lake City Central, ilikuwa ya kusisimua. Sikumjua mtu yeyote ambaye alikuwa ametumikia katika Jiji la Salt Lake. Nilidhani labda nilikuwa nimefungua wito usio sahihi wa misheni. Nilipofika Jijini Salt Lake, nilihisi kwamba kila kitu nilichojua kilikuwa kimeondolewa. Nilijikuta kwenye baiskeli kwenye theluji bila wazo lolote la jinsi ya kuwa mmisionari. Pamoja na utamaduni wake tofauti na hali ya hewa, Jiji la Salt Lake lilikuwa mbali sana na Afrika Kusini kwa kadiri ambavyo ningesafiri.

Katika eneo langu la kwanza, mimi na mwenzangu tulimtembelea muumini aliyeitwa Chris Ruppel kwa chakula cha jioni. Aliuliza ikiwa mmoja wetu alijua muziki. Mwenzangu alitaja kwamba nilicheza kinanda na kuimba, hivyo niliimba wimbo kwa ajili ya familia. Kisha kitu maalumu kilitokea. Kaka Ruppel alinitazama na kusema, “Mzee Vizzini, kama utaendelea kuimba kama hiyo, utakuwa mmisionari mwenye mafanikio.” Nilidhani alikuwa tu amelipenda jambo hilo lakini sikulifikiria sana.

Miezi michache baadaye, pamoja na Kaka Ruppel, nilisaidia kupanga mkutano wa wamisionari wa mafunzo ya muziki. Katika kila eneo nililotumikia baada ya hapo, tulitumia muundo huu wa mkutano wa mafunzo. Watu wengi walishiriki nasi, kutoka kwa waumini wa kigingi hadi kwa wanamuziki na waumini wa imani zingine. Tulifundisha kuhusu Mwokozi kupitia muziki kwa watu ambao vinginevyo wasingetaka kuketi katika somo zima. Nilijifunza kwamba muziki ungeweza kuwagusa wote masikini na matajiri, walioelimika na wasio na elimu.

Misheni yangu ilinifundisha kwamba ninaweza kufanya mambo magumu. Nilipotumikia katika eneo mbali sana na tofauti sana na nyumbani kwangu, nilijifunza kwamba kila mtu ni mtoto wa Mungu. Nimeona miujiza katika maisha ya watu upande mwingine wa dunia katika Utah, na nimeiona hapa Afrika Kusini. Ninajua kwamba kama tuna imani, miujiza inaweza kutokea katika maisha ya kila mmoja wetu (ona Mormoni 9:15–21).