2025
Fedha Haiwezi Kununua Furaha, lakini Kristo Anatoa Shangwe Bure
Januari 2025


“Fedha Haiwezi Kununua Furaha, lakini Kristo Hutoa Shangwe Bure,” Liahona, Jan. 2025.

Vijana Wakubwa

Fedha Haiwezi Kununua Furaha, lakini Kristo Anatoa Shangwe Bure

Wakati kushikilia fedha kwangu kulishinda vipaumbele vyangu, niligundua nilikuwa nikichagua ulimwengu juu ya Baba wa Mbinguni.

msichana mkubwa akiangalia kupitia dirisha la duka

Picha za mwandishi na Stephen Neilsen

Nilipokuwa nakua, nilikuwa na matamanio mengi. Niliwaona watu wa umri wangu tayari wakipata pesa na kupata mafanikio kwenye mitandao ya kijamii. Nilitaka niwe kama wao tu.

Nilipokuwa nikihudhuria chuo kikuu na kujifunza kuwa peke yangu, fedha ikawa kipaumbele changu cha juu. Yote niliyoyajali yalikuwa ni kustahili udhamini, kuweka akiba na kujiandaa kwa ajili ya kazi yangu ya baadaye.

Hata mipasho yangu ya mitandao ya kijamii ilijaa na jumbe kuhusu uzalishaji, kuwekeza, na kazi za kando ili kunisaidia kupata fedha za ziada. Nilikuwa na wasiwasi kwamba kama nisingechukua kila fursa kuwa mwerevu kwa fedha zangu, nisingekuwa salama kifedha.

Nilikumbatia utamaduni huu, nikifikiri ungenifanya niwe na furaha na mafanikio. Daima nilihalalisha fokasi yangu kwenye fedha kwa kujiambia kwamba siku moja, wakati nilipokuwa na pesa nyingi, ningeweza kutoa mchango zaidi kwa taasisi za msaada na kuwa mtu bora zaidi kwa njia hiyo.

Sikugundua wakati huo, lakini kadiri matamanio yangu ya fedha yalivyoshinda vipaumbele vyangu, nilianza kupoteza furaha maishani mwangu. Nilikuwa na ongezeko la wivu, hasa kwa wale walioonekana kuwa na zaidi ya fedha za kutosha.

Nilianza kutaka mafanikio zaidi kwenye mitandao ya kijamii, katika kazi yangu, na hata na jinsi watu wengine walivyoniona. Lakini ilionekana kama vile zaidi nilivyosaka mafanikio, ndivyo nilivyohisi kuwa na mafanikio kidogo—na ndivyo nilivyokuwa mbali na Baba wa Mbinguni.

Kutambua Kupenda Mali

Baada ya takribani mwaka mmoja wa hisia kama hii, nilikuwa nasikiliza hotuba ya Rais Dallin H. Oaks, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza. Nilihisi moyo wangu ukizama nilipokuwa nikimsikia akielezea hasa ni aina gani ya mtu niliyegeuka kuwa:

“Hata leo baadhi wanaokiri Ukristo wanavutiwa zaidi na mambo ya ulimwengu—mambo yanayoleta uzima duniani lakini hayatoi lishe kwa uzima wa milele.”

Ningefikiri ningeweza kuyapa kipaumbele vyote Mungu na fedha kwa wakati mmoja, lakini maneno ya Rais Oaks na utambuzi huu katika Mathayo 6:24 yalithibitisha kuwa ni kweli: “Hakuna mtu anayeweza kutumikia mabwana wawili: kwani ama atamchukia yule mmoja, na kumpenda mwingine; au vinginevyo atamshikilia yule mmoja, na kumdharau mwingine. Huwezi kumtumikia Mungu na Mali.”

Wakati akili yangu ilipofokasi kwenye vitu vya kimwili, niliona ni vigumu kuona uzuri wa injili. Sikuelewa jinsi ya kwenda kanisani na kusoma maandiko kungeweza kunisaidia katika malengo yangu.

Wakati kupata elimu zaidi na kupata mapato thabiti ni shughuli zinazostahili, nilikuwa nikizipa kipaumbele sana. Nilikuwa nimepitiliza. Nilitambua kwamba ningekuwa na huzuni hadi nilipojifunza kubadili mawazo yangu.

Kufokasi kwenye Kile Kilicho Muhimu Zaidi

Nilisali kwa Baba wa Mbinguni na kumuuliza kama angeweza kunisaidia kuanza kufokasi juu ya kile kilicho muhimu zaidi. Nilianza kwa kusoma maandiko. Nilipokuwa nikijifunza mistari ambayo nilidhani nimeisoma mara nyingi kabla, hadithi hizi za kawaida zilianza kuvuta usikivu wangu. Nilihisi Roho Mtakatifu akiwasiliana nami!

Hadithi moja ambayo ilinivutia ilikuwa ni ile ya kijana tajiri. Yesu alimwambia: “Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, na uwape maskini, na utakuwa na hazina mbinguni: kisha njoo unifuate” (Mathayo 19:21).

Niliposoma hadithi hii ya maandiko, nilihisi msukumo wa kutulia na kufikiria kuhusu jinsi hili lilivyotumika kwangu. Mwanzoni, haikuonekana kama nilikuwa na chochote kinachofanana na mtawala kijana tajiri—tayari alikuwa na utajiri wake na hakuwa tayari kuachana nao. Mimi, kwa upande mwingine, sikuwa tajiri, na nilidhani juhudi zangu za kupata fedha zaidi zilikuwa za haki.

Lakini punde nilitambua kwamba ilikuwa vigumu kwangu kutoa fedha zangu, kama vile mtawala kijana tajiri. Hususani ukizingatia kuwa nilikuwa tayari kwenye kuhangaika zaidi ili kupata fedha zaidi.

Nilitaka kumweka Baba wa Mbinguni kwanza katika maisha yangu tena. Niliamua kufungua shajara yangu, kuandika jinsi nilivyokuwa ninahisi, na kuangalia nyuma kwenye maingizo yangu ya awali ili kuelewa vyema kile kilichoanzisha tamaa yangu.

Nilipofanya hivi, nilikuwa na ufahamu zaidi wa jinsi vipaumbele vyangu vilivyobaki nyuma. Kama nilivyoona katika ingizo moja, “Ninaendelea kufikiria jinsi ninavyoweza kufaidika kutokana na kila kitu badala ya kufikiria kuhusu jinsi ninavyoweza kuwa bora au kuwasaidia wengine.”

Hatimaye, kwa kujifunza maandiko, kumsikiliza Roho, na kuandika shajara, nilianza kubadilika.

Kumtumaini Mungu badala ya Fedha

Imekuwa ya kustaajabisha kuhisi ahadi katika Mithali 3:5–6 ikitimia katika maisha yangu:

“Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usitegemee akili zako mwenyewe.

Katika njia zako zote mkiri Yeye, Naye Atayanyosha mapito yako.”

Bado ninajitahidi kukuza vipaji vyangu na kufanya kazi kwa bidii katika elimu yangu na kazi ya sanaa. Kutafuta usalama wa kifedha ili kujikimu wenyewe na familia zetu ni hamu ya haki. Hata hivyo, tunahitaji kuwa waangalifu tusiruhusu harakati zetu za mafanikio na fedha ziwe muhimu zaidi kuliko kitu kingine chochote.

Siku hizi, sijali kama ninakuwa maarufu au kutengeneza tani ya fedha kupitia sanaa wangu. Nimegundua kwamba kuishi maisha ninayopata kuyapenda—na kuhisi upendo kutoka kwa—Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, familia yangu na sanaa inatosha kwangu. Sikasirikii tena gharama zisizotarajiwa au mafanikio ya watu wengine. Badala yake, ninajitolea zaidi kwenye injili ya Yesu Kristo kwa sababu inaendelea kuniokoa kutokana na maisha ya uchoyo, kujilinganisha na kutoridhika kila mara. Na ninapoanza kusahau, maandiko na manabii daima hunikumbusha kile kilicho muhimu zaidi katika maisha.

Rais Russell M. Nelson alifundisha:

“Wakati ulimwengu unasisitiza kwamba nguvu, mali, umaarufu na starehe za kimwili ndizo ziletazo furaha, hazileti! Haziwezi kuleta!

“Ukweli ni kwamba inachosha sana kutafuta furaha mahali ambapo huwezi kamwe kuipata! Hata hivyo, unapojifunga mwenyewe nira kwa Yesu Kristo na kufanya kazi ya kiroho inayohitajika kuushinda ulimwengu, Yeye na ni Yeye pekee, aliye na uweza wa kukuinua juu ya mvuto wa ulimwengu huu.”

Kuushinda Ulimwengu

Mabadiliko ambayo Mwokozi amenisaidia kufanya katika nafsi yangu yamekuwa ya kimiujiza. Ninajua sasa kwamba mafanikio si kuhusu kuthibitisha jinsi ninavyopendeza au kuhusiana na thamani yangu kwa kiasi gani cha fedha ninachopata; ni kuhusu kuhisi shukrani kwa fursa ya kupata uzoefu wa maisha ya duniani na kuona baraka za kupendeza ambazo Baba wa Mbinguni daima amenipatia. Ninajua kama nitamweka Yeye kwanza, kila kitu kingine kitakaa katika sehemu yake.

Ninawahimiza mfikirie vipaumbele vyenu katika maisha. Je, umefokasi kwenye mali na kile ambacho huna? Au unafokasi kwenye kile kilicho muhimu zaidi? Kuwa mwaminifu kwako mwenyewe. Ona kama unahitaji kurekebisha njia yako ya kurudi kwa Mwokozi.

Unapofanya uchaguzi huo, utapata furaha zaidi kuliko ulivyowahi kufikiria inawezekana.