“Kanisa la Yesu Kristo la Urejesho,” Liahona, Jan. 2025.
Kutumia Majarida ya Kanisa
Kanisa la Yesu Kristo la Urejesho
Mafunzo ya Njoo, Unifuate ya mwaka huu ya Mafundisho na Maagano yataonyesha jinsi Bwana alivyorejesha Kanisa Lake na injili Yake kupitia manabii wa siku za mwisho. Makala nyingi katika toleo la mwezi huu zinaonyesha baraka za Urejesho.
Kujifunza kutoka kwenye Toleo Hili
Shiriki katika Kukusanyika.
Kwenye ukurasa wa 2, Rais Russell M. Nelson anashiriki njia tunavyoweza kukusanyika kwa Mwokozi, kukusanyika na Watakatifu, na kukusanyika katika huduma ya Mungu. Fikiria kuweka lengo la mwezi huu ili kuchangia mojawapo ya aina hizo tatu za kukusanyika.
Tumikia katika Kanisa la Urejesho
Mzee Patrick Kearon wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili anazungumza kuhusu fursa tulizonazo katika Kanisa la Yesu Kristo la urejesho za “kuwatumikia wengine kwa upendo” (ona ukurasa wa 8). Je, kuna watu katika kata au tawi lako ambao wanasumbuka? Ungeweza kuwaombea watu hawa na kuomba mwongozo wa kiungu juu ya jinsi ya kuwahudumia.
Jifunze kutoka kwenye Tangazo la Urejesho
Mnamo 2020, Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili walitoa “Urejesho wa Utimilifu wa Injili ya Yesu Kristo: Tangazo kwa Ulimwengu la Miaka Mia Mbili” (ona ukurasa wa 40). Unaporejelea tangazo la Urejesho, unaweza kufikiria maswali haya: Ni matukio gani muhimu yanayotajwa, na ni kwa jinsi gani Bwana aliongoza matukio hayo?
Kutoka Jarida la Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Urais Mkuu wa Wasichana na Wavulana na wengine wanatambulisha dhima ya mwaka huu.
Tunaweza kujifunza nini kutokana na maelezo tofauti ya Joseph Smith ya Ono lake la Kwanza?
Ona baadhi ya matukio makubwa ya Urejesho wa injili ya Yesu Kristo unaoendelea.
Kipande cha karatasi kinaweza kuwasaidia vijana kuona jinsi kumwamini Mungu ni njia bora zaidi wakati imani yao inapopingwa au wanakabiliana na maswali yanayochanganya.
Kutoka kwenye Jarida la Rafiki
Wasaidie watoto wako watengeneze kitu cha ufundi ili kujifunza kuhusu Joseph Smith na Urejesho.
Tengeneza pishi lenye afya ili kufurahia pamoja na familia yako na kuitunza miili yenu.
Soma kuhusu msichana aliyehisi upendo wa Mungu ingawa maombi yake hayakujibiwa jinsi alivyotaka.
Angalia mfululizo mpya kuhusu historia ya Kanisa na Mafundisho na Maagano, ukianza na Ono la Kwanza.