Karatasi “Isiyowezekana”
Ninaweza kukata tundu la kutosha la mimi kupita kwenye kipande cha kawaida cha karatasi. Huniamini? Unadhani haiwezekani? Ninaahidi, sio hila. Unaweza kutumia somo hili la vitendo kufundisha darasa lako, akidi, au familia yako kuhusu kumtumainia Mungu wakati una maswali—hata “yasiyowezekana”.
-
Uliza kundi lako kama wanaamini unaweza kukata tundu katika kipande cha karatasi ambalo ni kubwa vya kutosha mtu kupita. Majibu ni kwamba, baadhi hawatakuamini.
-
Soma Joseph Smith—Historia 1:23–25. Elezea kwamba watu wengi hawakuamini inawezekana kwamba Joseph Smith ameona ono. Lakini yeye alijua ilikuwa ni kweli.
-
Muda wa kukata tundu!
-
Kunja karatasi nusu mbili zinazolingana.
-
Anza kukata kwenye mkunjo, kata wima kila mwisho wa karatasi, lakini sitisha kabla ya kufikia ukingo.
-
Zungusha nyuma na mbele kutoka upande mmoja hadi mwingine, endelea kukata vipande vya wima ndani ya karatasi (bila kukata hadi mwisho!).
-
Ukiruka juu ya kingo za vipande viwili , kata kando ya mkunjo wa karatasi.
-
Ikunjue, na hapo unalo—tundu kubwa la kutosha kupita!
-
-
Jadili jinsi gani kwa sababu tu kitu kinakanganya au kinaonekana hakiwezekani, hiyo haimaanishi kwamba si kweli. Joseph Smith aliwaona Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Kunaweza kuwa na nyakati ambapo imani yako inapingwa na wengine, au unakutana na maswali ya kukanganya. Wakati hili linapotokea, fikiria kuhusu karatasi “isiyowezekana”. Amua kumtumaini Mungu na kumgeukia Yeye na vyanzo vingine vizuri kwa ajili ya majibu.
Imani ni kuwa na tumaini kwa mambo ambayo hayaonekani lakini ni ya kweli. Tilia shaka mashaka yako kabla ya kutilia shaka imani yako.”