Dhima ya Vijana kwa Mwaka 2025
Njia 7 za Kumtegemea Kristo
Jaribu tabia hizi ili kuweka macho yako juu ya Mwokozi.
Kutumia dhima ya vijana kwa mwaka huu—“Mtegemee Kristo”—kidogo huleta changamoto. Ni kwa jinsi gani unamtegemea mtu ambaye hayupo kimwili? Anza na tabia hizi saba.
1. Kumbuka Kwamba Yeye Hajifichi
Ndio, unatakiwa kumtafuta Yeye. Lakini Anataka kutafutwa! Sio mchezo wa kujificha-na-kutafuta. Bwana ana hamu ya kukubariki—kwa kweli, inamfurahisha Yeye (ona Mafundisho na Maagano 41:1). Hatafuti sababu za kukuzuia. Kinyume kabisa: Yeye daima anatafuta kukubariki. Kama Mzee Patrick Kearon wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alivyofundisha, “La, [Mwokozi] haweki vizuizi barabarani na vipingamizi; Yeye huviondoa. Hakuachi nje; Yeye anakukaribisha ndani. Huduma Yake yote ilikuwa ni tangazo hai la nia hii.
2. Kiri Ushawishi Wake katika Maisha Yako
Bwana anaridhika wakati “tunapokiri … mkono wake katika mambo yote” (Mafundisho na Maagano 59:21). Kwa hivyo hakikisha unatambua ushawishi Wake katika maisha yako! Mshukuru Yeye wakati mambo yanapokwenda vyema kwa ajili yako na tafuta amani na uelewa wakati yasipokuendea vyema.
3. Kuwa mwenye Shukrani kwa Kile Ulichonacho
Pamoja na kutambua ushawishi wa Bwana katika maisha yako, ni muhimu pia kuhisi—na kuonyesha—shukrani. Unaweza usimwone Mwokozi kimwili, lakini unaweza kuona baraka Zake katika maisha yako! Mzee Gary B. Sabin wa Wale Sabini alisema, “Kamwe hutakuwa na furaha kuliko unavyoshukuru.” Mshukuru Bwana kila siku kwa baraka zako. Unapohisi kulemewa, fuata ushauri wa wimbo wa zamani: “Hesabu baraka zako; zihesabu kwa moja moja, na itakushangaza kile ambacho Bwana amefanya.”
4. Sali Kila Siku
Utaweza vizuri zaidi “kumwona” Mwokozi siku nzima ikiwa utaanza kwa kuzungumza na Baba wa Mbinguni. Muombe Yeye akusaidie kumkumbuka Mwokozi na kugundua ushawishi Wake katika maisha yako. Unaweza kusali kila mara kadiri unavyotaka wakati wa mchana. Na kabla ya kulala, sali tena kumwambia Baba wa Mbinguni jinsi mambo yalivyokwenda. Kamwe hachoki kusikia kutoka kwako!
5. Kukariri Maandiko na Nyimbo za Dini
Njia moja ya kuweka mawazo yako ukifokasi kwa Yesu Kristo ni kuwa na maneno ya maandiko unayoyapenda au maneno ya wimbo wa kuinua katika kumbukumbu yako. Fanya mazoezi ya kuzikumbuka wakati unapohisi mawazo hasi yakiingia. Mara nyingi tukikumbuka (na kuimba kimya kimya) kichwa cha wimbo kinaweza kuwa cha kutosha kuelekeza upya mawazo yako: “Mimi mwana wa Mungu.” Nina Haja Nawe Kila Saa, “Tulia nafsi yangu.”
6. Angalia Picha za Mwokozi
Tafuta baadhi ya picha za sanaa za Mwokozi ambazo unazipenda, na kisha ziweke mahali ambapo utaziona mara kwa mara. Baadhi ya maeneo yanaweza kujumuisha ukuta wa chumba chako cha kulala, kioo chako cha bafuni, kabati yako ya shule, au kama usuli kwenye kompyuta yako au skrini ya simu yako.
7. Angalia Ulimwengu Unaokuzunguka
Ni mzuri Na Mwokozi aliuumba huo kwa ajili yako (ona Mafundisho na Maagano 14:9)! Hakuna sababu tuijuayo ya kwa nini dunia ilibidi iwe ya kupendeza. Pengine tungeweza kuishi maisha ya duniani katika dunia ambayo ilikuwa tambarare, mraba, na kijivu. Badala yake Mwokozi aliumba ulimwengu “kwa faida na matumizi ya mwanadamu, ili kuridhisha jicho na kufurahisha moyo” (Mafundisho na Maagano 59:18). Kwa maneno mengine, dunia ni nzuri kwa sababu vitu vizuri hutufanya tujisikie vizuri. Kama unataka kumkumbuka Mwokozi, angalia kuzunguka ulipo.