Unganika
Ivan B.
17, Zagreb, Croatia
Picha na Ashlee Larsen
“Mimi ni muumini pekee wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho katika shule yangu. Wakati mmoja kwenye sherehe ya kuzaliwa, marafiki zangu walianza kunywa vilevi. Nilijisikia vibaya na kwenda nyumbani. Waliponiuliza kwa nini niliondoka mapema, nilisema mimi sinywi vilevi na sikuwa na faraja. Hawakupenda jibu hilo na hivyo walichukia. Lakini baada ya muda, marafiki zangu kwa kiasi fulani wamelikubali.
Wakati mwingine, mwalimu wangu aliniomba nishiriki onyesho la PowerPoint kuhusu Kanisa. Wengi wa wanadarasa wenzangu walikuwa na maswali, na nilihisi kama Yesu Kristo alikuwa akifundisha kupitia mimi. Unaposhiriki ushuhuda wako, huna haja ya kuogopa kile wengine wanachofikiria. Kama unamwamini Bwana, Yeye atakusaidia kujua nini cha kusema.
Ninataka kwenda misheni ili niweze kuwaleta watu wengine kwa Kristo. Ninaamini kwamba Mwokozi alijichukulia juu Yake mwenyewe dhambi za ulimwengu. Tunaweza kukusanya Israeli na kumwalika kila mtu kuja Kwake.