2025
Yanafanana Zaidi Kuliko Unavyofikiria
Januari 2024


Yanafanana Zaidi Kuliko Unavyofikiria

mama na mwana

Andy. Habari za shule?

Nzuri. Tulizungumza kuhusu dini tofauti. Nilijifunza mengi kuhusu imani zingine—tunayo mengi yanayofanana kuliko nilivyofikiria!

mama akizungumza

Lo! Ulijifunza nini?

Mwanamke Muislamu anasali

Nilijifunza kwamba Ayla ni Muislamu, na anasali mara tano kwa siku.

mvulana akiimba kanisani

Stefano ni Mbaptisti, na ana msifu Mungu wakati anapokwenda kanisani.

Mwanamke Mkatoliki akisali

Anastasia ni Mkatoliki. Anatubu kupitia sala na kuungama.

Wayahudi wakitembea kutoka kwenye sinagogi

Na Lawi ni Myahudi. Familia yake inafuata sheria za Mungu za kuongoza maisha yao.

mama akizungumza

Lo!, ulijifunza mengi! Je, ulishiriki chochote na darasa lako?

mvulana akiwa ameshikilia picha ya Yesu Kristo

Ndiyo! Niliwaambia kwamba Yesu Kristo ananijua na ananipenda, na kwamba ninajaribu kuwa kama Yeye.