2025
Urejesho Unaoendelea
Januari 2024


UrejeshoUnaoendelea

Ukengeufu Mkuu

magofu

Vielelezo na Katy Dockrill

Watu wanageuka dhidi ya Mwokozi na Mitume Wake. Kanisa linaanguka kwenye uharibifu wa kiroho na halipo tena duniani.

njia msituni

1820

Ono la Kwanza Mungu Baba na Yesu Kristo wanamtokea Joseph Smith mwenye umri wa miaka 14.

Malaika Moroni na mabamba ya dhahabu

1823

Malaika Moroni anamtokea Joseph Smith, akimwambia kuhusu mabamba ya dhahabu.

Cheti

1829–1830

Ukuhani wa Haruni na Ukuhani wa Melkizedeki unarejeshwa.

Joseph Smith anatafsiri Kitabu cha Mormoni (karibu ndani ya miezi mitatu!), na kinachapishwa.

Kanisa linaanzishwa rasmi, mnamo Aprili 6, 1830.

waumini rasmi 6 wa mwanzo; punde baadaye, 280

Mitume

1835–1836

Akidi ya Mitume Kumi na Wawili inaanzishwa

Kitabu cha Mafundisho na Maagano kinachapishwa

Mwokozi, Musa, Elia, na Eliya wanatokea katika Hekalu la Kirtland na kurejesha funguo za ukuhani (ona Mafundisho na Maagano 110).

Zaidi ya waumini 13,000

Hekalu 1

Gazeti

1840–1842

Ubatizo kwa niaba ya wafu unafundishwa hadharani.

Muungano wa Usaidizi unaanzishwa.

Endaumenti kamili ya kwanza ya hekaluni inatolewa.

1869–1880

Programu za Wasichana na Wavulana za mwanzo zinaanzishwa.

Kitabu cha Lulu ya Thamani Kuu kinakubaliwa kama kitabu kitakatifu.

Zaidi ya waumini 133,000

Hekalu 1

1936

Programu ya awali ya ustawi wa Kanisa inaanza.

Zaidi ya waumini 760,000

Mahekalu7

watu wakiwa wameshikana mikono nje ya hekalu

1978

Ibada za hekaluni zinazotolewa kwa waumini watu wazima wote wenye kustahili, na kutawazwa katika ukuhani kwa wanaume wote wenye kustahili kunaidhinishwa.

Zaidi ya waumini milioni 4

Mahekalu 17, ikijumuisha Uswisi, New Zealand, Uingereza, na Brazil

Tangazo

1995

“Familia: Tangazo kwa Ulimwengu linatolewa.

Zaidi ya waumini milioni 9.25

Mahekalu 47, yaliyotawanyika zaidi ya mabara 6

beji za majina ya wamisionari

2012

Umri wa misheni umeshushwa kutoka 19 hadi 18 kwa wanaume na kutoka 21 hadi 19 kwa wanawake.

Zaidi ya waumini milioni 14.5

Mahekalu 140

hekalu na saa

2018–2020

Vijana wanapewa fursa pana za kuhudumu hekaluni.

Ratiba ya Kanisa Jumapili inafupishwa kutoka masaa 3 hadi 2.

Zaidi ya waumini milioni 16.5

Mahekalu 168

Ulimwengu

2025

Urejesho bado unaendelea! Kuna waumini wa Kanisa katika zaidi ya nchi na mipaka ya kijiografia 200, wakizungumza zaidi ya lugha 700!

Kuanzia Aprili 2024: mahekalu 189 yaliyowekwa wakfu, 161 zaidi yalitangazwa (jumla 350).

Zaidi ya waumini milioni 17.25