2025
Liège, Ubelgiji
Januari 2025


“Liège, Ubelgiji,” Liahona, Jan. 2025

Kanisa Liko Hapa

Liège, Ubelgiji

ramani ya ulimwengu ikiwa na duara kuzunguka Ubelgiji
majengo karibu na mto

Injili ya urejesho ya Yesu Kristo yawezekana iliwasili kwa mara ya kwanza nchini Ubelgiji wakati mwongofu wa Watakatifu wa Siku za Mwisho kutoka Uturuki, Mischa Markow, alianza kufundisha familia ya Esselman mwaka 1888. Baada ya wao kubatizwa, wamisionari nchini Uswisi na Ujerumani walianza kutumikia nchini Ubelgiji. Katika miezi miwili, watu 80 walijiunga na Kanisa, na mikusanyiko ilianzishwa huko Liège, Brussels na Antwerp. Leo, Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho lina:

  • Waumini 6,600 (kwa makadirio)

  • Vigingi 2 (kata 11, matawi 2)

  • Hekalu 1 (lililotangazwa mwaka 2021, litakalojengwa Brussels)

Baraka za Kujifunza Maandiko

Karen Wery wa Kata ya Namur anasema kuhusu familia yake: “Tunajifunza maandiko yetu pamoja na kushiriki mawazo yetu na maongozi kwa kila mmoja wetu. Tunatumia maandiko lakini pia video na nyenzo zingine, kama vile jarida la Rafiki, kuwasaidia watoto wetu kuelewa vyema mafundisho. Jambo kubwa tulilokuwa nalo ni ukuaji wa umoja katika nyumba yetu.”

Familia ya Wery