2025
Kuijenga Nauvoo
Mei 2025


“Kujenga Nauvoo,” Rafiki, Septemba 2025, 26–28.

Hadithi za Maandiko

Kuijenga Nauvoo

Watakatifu wa mwanzo wanaoishi katika mahema kando ya kingo za Mto Mississippi

Bwana aliwaambia Watakatifu kukusanyika katika sehemu mpya. Ilikuwa karibu na mto mkubwa, ambapo nchi ilikuwa imelowa maji na matope. Haikuonekana kama mahali pazuri pa kujenga mji. Lakini Nabii Joseph Smith alijua kwamba kwa msaada wa Bwana, wangeweza kuifanya iwe nzuri.

Mtu akiwa amebeba mbao kwenye bega lake, farasi na mkokoteni pamoja na vifaa vya ujenzi, na vibanda vya magogo
Joseph Smith na wanaume wengine wakiweka matofali wanapojenga nyumba

Watakatifu walifanya kazi kwa bidii ili kupafanya mahali pazuri pa kuishi. Joseph aliuita mji wa Nauvoo, ambao unamaanisha “mahali pazuri.”

Joseph Smith akionyesha eneo mlimani kwa ajili ya hekalu

Bwana alitaka Watakatifu Wake kujenga hekalu huko Nauvoo. Watu haraka walianza kufanya kazi.

Joseph Smith akiwafundisha Watakatifu wengine katika nyumba

Bwana alikuwa na baraka kuu za kuwapa watu Wake. Hekaluni, wangefanya maagano, au ahadi maalumu, na Bwana. Pia wangejifunza kuhusu mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni kwa ajili ya watoto Wake wote.

Hekalu la Nauvoo lililomalizika

Watakatifu walifanya kazi kwa bidii ili kujenga hekalu. Ilichukua muda mrefu, lakini walikuwa na shauku ya kujifunza kuhusu ahadi maalumu ambazo Bwana alikuwa nazo kwa ajili yao katika hekalu Lake.