“Shughuli zaNjoo, Unifuate,” Rafiki, Septemba 2025, 22–23.
Shughuli za Njoo Unifuate
Septemba 1–7: Mafundisho na Maagano 94–97
Jenga Hekalu
Hekalu ni mahali ambapo Mungu anaweza kutubariki ( ona Mafundisho na Maagano 95:8). Jenga hekalu lako mwenyewe kwa kutumia michemraba ya sukari, matofali au vitu vya asili! Kisha tutumie picha ya ubunifu wako! Geuza kwenye jalada la nyuma ili uone jinsi ya kufanya hivyo.
Septemba 8–14: Mafundisho na Maagano 98–101
Tulia
Maandiko yanafundisha, “Tulieni na jueni kuwa Mimi ni Mungu” (Mafundisho na Maagano 101:16). Hiyo inamaanisha kwamba tunapochukua muda wa kuwa wanyenyekevu, tunaweza kuhisi kuwa karibu na Baba wa Mbinguni. Cheza mchezo huu kuhusu kutulia. Mtu mmoja anakimbia na kujaribu kumtagi mtu mwingine. Wakati mtu anapokuwa ametagiwa, wanasimama kwa utulivu sana. Kabla hawajaweza kukimbia tena, wanasema jambo moja wanalolijua kuhusu Baba wa Mbinguni.
Septemba 15–21: Mafundisho na Maagano 102–105
Sanaa ya Mshumaa
Tunaweza kuwa nuru kwa wengine kwa kufuata mfano wa Yesu Kristo na kuwatumikia wengine (ona Mafundisho na Maagano 103:9). Geuza kwenye ukurasa wa 13 kutengeneza sanaa ya mshumaa.
Septemba 22–28: Mafundisho na Maagano 106–108
Shughuli za Mkutano Mkuu
Ni muhimu kumsikiliza nabii na mitume wa Mungu (ona ona Mafundisho na Maagano 107:22–23). Soma hadithi kwenye ukurasa wa 4 kuhusu kupata majibu kutoka kwenye mkutano mkuu. Andika baadhi ya maswali yako mwenyewe kwenye ukurasa wa 6. Utapata pia shughuli unazoweza kufanya wakati unaposikiliza mkutano.
Picha na Christina Smith