2025
Ushuhuda wa Muziki
Mei 2025


“Ushuhuda Wangu wa Muziki,” Rafiki, Septemba 2025, 19.

Imeandikwa na Wewe

Ushuhuda Wangu Wa Muziki

Msichana amekaa kwenye dawati darasani akiwa na mtawa wa Kikatoliki akiwa amesimama mbele ya chumba

Katika nchi yangu, watu wengi ni Wakatoliki. Ninaenda katika shule ya Kikatoliki.

Nilipokuwa darasa la pili, mwalimu wangu alicheza muziki wakati tukifanyia kazi shughuli zetu za siku. Mchana mmoja, aliuliza kama mtu yeyote alitaka kuchagua wimbo wa kusikiliza. Nilikuwa nafikia miaka minane mwaka huo na nilikuwa nikijiandaa kwa ajili ya ubatizo wangu. Maneno “Napenda kutafuta upinde wa mvua” yalinijia akilini mwangu. Nilimwomba mwalimu wangu kupiga wimbo “When I Am Baptized” kutoka Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Mwalimu wangu alikubali na kuutafuta.

Punde wimbo ulipigwa kwa ajili ya kila mtu darasani kwangu kusikia. Mwanzoni baadhi ya wanadarasa wenzangu walinitazama kwa ajabu, lakini baadaye niliweza kumhisi Roho Mtakatifu moyoni mwangu. Alinijaza amani.

Siku ile nilipoondoka shuleni, nilihisi furaha sana kwamba nilikuwa nimeshiriki injili pamoja na wanadarasa wenzangu kupitia wimbo wangu ninaoupenda wa Msingi. Nadhani ilikuwa ni njia nzuri ya kuniandaa kuwaalika marafiki zangu kwenye ubatizo wangu.

Ukurasa wa PDF

Kielelezo na Simini Blocker