2025
Nifundishe Kuhusu Baraka za Ukuhani
Mei 2025


“Nifundishe Kuhusu Baraka za Ukuhani,” Rafiki, Sept. 2025, 46–47.

Misingi ya Injili

Nifundishe Kuhusu Baraka za Ukuhani

Wanaume wawili wakimpa baraka msichana mgonjwa kitandani

Ukuhani ni nguvu ya Mungu hapa duniani. Tunaweza kupata baraka ya ukuhani tunapokuwa wagonjwa ili kutusaidia kuhisi vizuri zaidi.

Mwanaume akimfariji msichana mdogo

Baraka inaweza kutufariji wakati tunapokuwa na hofu au huzuni.

Mtu akimpa mvulana baraka; mwanamke amekaa karibu akiwa amebeba mtoto; mvulana ameweka begi la mgongoni karibu na kiti chake

Baraka inaweza kutusaidia kuhisi ujasiri kabla ya kitu fulani muhimu.

Mwanaume anayetabasamu akiwa amembeba mwanawe mdogo anayetabasamu

Tunaweza kuomba baraka ya ukuhani wakati wowote!

Paka Rangi Picha.

Unaweza kupata baraka maalumu ya ukuhani unapokuwa mtoto mchanga. Paka rangi picha hapo chini

Ukurasa wa PDF

Vielelezo na Audrey Day