“Kwa Ajili ya Watoto Wadogo,” Rafiki, Septemba 2025, 42–43.
Kwa Ajili ya Watoto Wadogo
Ninampenda Yesu kwa sababu Yeye ni mkarimu.
Malhia M., umri miaka 3, Liège, Ubelgiji
Ninampenda Yesu kwa sababu Anatupenda na alijitoa dhabihu Kwa ajili yetu.
Gauthier M., umri miaka 5, Liège, Ubelgiji
Tafuta Hekalu
Msaidie mvulana kufika hekaluni huko Nauvoo. Watafuteni marafiki zake njiani!
Fuatilia Maumbo
Watoto wa Norway wanasoma Kitabu cha Mormoni kwa lugha ya kinorweyi. Chora kwenye mistari ili kumalizia picha.
Ni Wewe!.
Sisi ni watoto wa Baba wa Mbinguni, na Yeye alitufanya sote tofauti. Paka rangi uso ili uonekane kama wewe!
Vielelezo na Katie Rewse