2025
Nguvu za Mungu Ni Kipawa!
Mei 2025


“Nguvu za Mungu Ni Zawadi!” Rafiki, Septemba 2025, 20–21.

Nguvu za Mungu Ni Kipawa!

Imetoholewa kutoka “Ishi Kulingana na Fursa Zako,” Liahona, Nov. 2024, 7–10.

Emma Smith akiwa amekaa ndani ya kibanda cha magogo akiwa ameshikilia kikombe cha chuma

Hivi karibuni nilitembelea Harmony, Pennsylvania, Marekani. Huko, chini ya miti ya maple, ukuhani ulirejeshwa kwa Joseph Smith na Oliver Cowdery. Pia nilienda nyumbani ambapo Joseph na Emma Smith waliishi. Ndani, nilisimama dirishani na kujiuliza kile Emma alifikiria wakati alipotazama kupitia dirisha hilo.

Bwana alimpa Emma ujumbe muhimu kupitia nabii Wake, Joseph. Tunaweza kusoma ujumbe huu katika Mafundisho na Maagano 25.

Kwanza, Bwana alimfundisha Emma kwamba alikuwa na nafasi katika mpango Wake. Alimkumbusha kwamba alikuwa binti katika ufalme Wake.

Pili, Bwana alimpa madhumuni. Emma alifanya sehemu muhimu ya Urejesho. Aliombwa kufundisha maandiko na kutengeneza kitabu cha kwanza cha nyimbo za kanisa!

Mwisho, Bwana alimfundisha Emma kuhusu maagano yake. Kushika maagano kungemsaidia kuhisi Roho, kuwa bora na kupokea maelekezo kwa ajili ya maisha yake.

Mvulana na msichana wamekaa katika kiti cha kanisa wakishiriki mkate wa sakramenti

Tumaini langu ni kwamba mtajifunza jinsi ibada za ukuhani na ahadi za maagano zitaruhusu nguvu ya Mungu katika maisha yako. Sisi sote tunaweza kufikia kipawa cha nguvu za Mungu. Kila wakati tunaposhiriki sakramenti. Kila wakati tunapoingia hekaluni.

Muziki wa Mchezo wa Kurusha

Emma Smith aliombwa kutengeneza kitabu cha kwanza cha nyimbo za kanisa. Bado tunaimba nyimbo za kanisa leo! Fanya zamu kurusha sarafu au kitu kingine kidogo kwenye ubao. Inapotua kwenye picha, fikiria wimbo kuhusu mada hiyo. Kisha imbeni pamoja!

Ukurasa wa PDF

Vielelezo na Shawna J. C. Tenney