2025
Kucheza Pamoja
Mei 2025


“Kucheza Pamoja,” Rafiki, Septemba. 2025, 44–45.

Msomaji wa Haraka

Kucheza Pamoja

Hadithi ya kweli kutoka Marekani.

Diego alikuwa mpweke. Familia yake ilikuwa imehamia mahali papya. Aliwakumbuka rafiki zake kutoka makazi yake ya zamani.

Mvulana akionekana mwenye huzuni anapocheza na dada yake mdogo

Diego alicheza na dada yake mdogo Cara. Lakini pia alitaka rafiki mpya.

Mwanaume na mwanamke wakiwatambulisha wana wao

Punde familia ilihamia mlango unaofuatia. Walikuwa na mvulana mdogo, kama vile yeye! Jina lake lilikuwa Sam.

Diego na Sam walicheza pamoja kila siku.

Mvulana akicheza na treni za wanasesere; mvulana akimfariji dada yake mdogo anayelia

Siku moja wakati wakicheza, Diego aliona kwamba Cara alikuwa na huzuni. Pengine Yeye alikuwa mpweke pia.

Mvulana mwenye tabasamu na msichana mwenye furaha wakitandaza mikono yao

“Je, unataka kucheza nasi?” Diego aliuliza.

Cara alitoa tabasamu bashasha. “Cheza!”

Wavulana wawili na msichana wakicheza na treni za mwanasesere pamoja

Diego, Sam na Cara walicheza mchezo wa treni pamoja. Walisukuma magari ya treni ya mwanasesere nyuma na mbele. “Choo-choo!” Diego alitabasamu. Alikuwa na burudani, na vivyo hivyo Cara!

PDF ya hadithi

Vielelezo na Natalie Briscoe