2025
Kumfuata Yesu huko Puerto Rico
Mei 2025


“Kumfuta Yesu huko Puerto Rico,” Rafiki, Septemba. 2025, 10–11.

Kumfuata Yesu huko Puerto Rico

Kutana na Darieli

Mvulana mwenye kutabasamu

Dariel anamfuata Yesu kwa kusoma maandiko na kusali. Anasema, “Ninapenda kumfuata Yesu kwa kujifunza zaidi kumhusu Yeye.”

Darieli pia anajaribu kumfuata Yesu kwa kuwatumikia wengine. Yeye humsaidia mwalimu wake kwa kusafisha kompyuta mpakato baada ya darasa. Anahudumia familia yake kwa kutunza wanyama wao wa kufuga na kusaidia kutengeneza chakula cha jioni. “Ninahisi furaha ninapomfuata Yesu,” alisema.

Kuhusu Darieli

Mvulana pamoja na baba yake na paka wawili

Umri: miaka 9

Kutoka: Caguas, Puerto Rico

Lugha: Kispanishi, Kiingereza

Malengo: 1) Kuwa mmiliki wa biashara. 2) Msanifu michezo ya video.

Mambo ayapendayo : Kucheza michezo ya video na kuendesha baiskeli yake

Familia: Dariel, mama, baba, kaka, dada

Mvulana pamoja na baba yake, mama, kaka mkubwa na dada mdogo
Mvulana akicheza mchezo na dada yake mdogo na baba yake

Mambo Ayapendayo Darieli

Mvulana akisoma maandiko

Hadithi ya Maandiko: Wakati Yesu Kristo alipofufuka

Sikukuu: Krismasi

Chakula: Arroz con habichuelas (wali na maharagwe)

Tunda na mboga: Stroberi na viazi vitamu

Rangi: Nyeupe, nyeusi, nyekundu

Wimbo wa Watoto:When I Am Baptized” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 103)

Ukurasa wa PDF