2025
Swali la Lou la Mkutano
Mei 2025


“Swali la Lou la Mkutano,” Rafiki, Septemba 2025, 4–5.

Swali la Lou la Mkutano

“Je, napaswa kwenda kwenye tafrija ya Alice?” Lou aliandika.

Hadithi ya kweli kutoka Ubelgiji.

Msichana anayenuna akiangalia mwaliko wa tafrija

Lou alihisi msisimko alipokuwa akifungua bahasha ya buluu. Rafiki yake wa dhati Alice alikuwa na tafrija ya siku ya kuzaliwa, na alialikwa!

Lakini Lou aliposoma mwaliko, moyo wake ulizama. Sio tafrija nyingine siku ya Jumapili, aliwaza.

Familia ya Lou hawaendi kwenye tafrija siku za Jumapili. Badala yake, walitumia muda pamoja, walienda kanisani, na kufanya mambo mengine kumkumbuka Mwokozi.

Lakini tafrija hii ilikuwa vigumu sana kusema hapana. Jinsi gani angeweza kukosa siku ya kuzaliwa ya rafiki yake bora?

“Siwezi tu kwenda mara hii moja?” Lou aliwaomba wazazi wake usiku huo. “Ninajua Jumapili ni muhimu. Lakini sitaki kuikosa.”

“Ni uchaguzi mgumu,” Baba alisema. “Baba wa Mbinguni anatuomba tuifanye Jumapili kuwa siku takatifu. Lakini ni juu yako kuamua jinsi utakavyofanya.”

Mama alimkumbatia Lou. Mkutano mkuu ni mwisho wa wiki hii. Labda hili linaweza kuwa swali unalouliza.”

Familia ya Lou ilikuwa na desturi ya kuandika swali walilokuwa nalo kabla ya mkutano. Kisha wakati wa mkutano, walisikiliza majibu.

Lou aliguna kimya kimya. “SAWA.”

Msichana akiwa amepiga magoti kando ya kitanda chake na kusali; daftari na penseli viko kitandani mwake

Wakati wa kulala, Lou aliandika swali lake. Kisha alisali. “Baba wa Mbinguni, kwa kweli nataka kwenda kwenye sherehe hii, na sijui nini cha kufanya. Je, utanisaidia tafadhali kupata majibu ninapotazama mkutano mkuu?”

Watoto wamekaa kwenye kochi na wakiangalia kompyuta mpakato juu ya meza mbele yao

Siku chache baadaye, Lou na kaka zake walirundikana kwenye kochi. Ulikuwa wakati wa mkutano! Lou alichora katika daftari lake wakati wa wimbo wa ufunguzi. Kisha mnenaji wa kwanza akaanza.

Lou alitazama juu. Msemaji alikuwa akizungumza kuhusu siku ya Sabato! Alisema kwamba Mungu aliwabariki wale wanaotii amri Zake, hata kama baraka haikuja mara moja.

“Nadhani Baba wa Mbinguni tayari alijibu swali langu,” Lou alisema. Hiyo ilikuwa haraka!”

Wasichana wawili wakizungumza

Siku iliyofuata shuleni, Lou alimtafua Alice wakati wa mapumziko. “Asante kwa kunialika kwenye tafrija yako,” Lou alisema. Alivuta pumzi kwa nguvu. “Jumapili ni siku maalumu kwa ajili yangu mimi, na familia yangu. Kwa hiyo sitaweza kuja.”

“SAWA,” alisema Alice “Ninasikitika utaikosa.”

“Mimi pia,” alisema Lou. “Lakini siku ya Jumamosi, ungependa kwenda nami kwenye uwanja wa wanasarakasi? Kisha bado tunaweza kucheza pamoja na kusherehekea siku yako ya kuzaliwa.”

Napenda tufanye hivyo!” Alice alitabasamu.

Lou alitabasamu pia. Kutokwenda kwenye tafrija lilikuwa chaguo gumu la kufanya. Lakini alijua kilikuwa kitu sahihi. Na alikuwa na shukrani kwamba Baba wa Mbinguni alijibu swali lake muhimu.

PDF ya hadithi

Vielelezo na Flavio Remontti