“Mambo 5 ya Kukumbuka kuhusu Usalama wa Mwili,” Rafiki, Septemba 2025, 38–39.
Mambo 5 ya Kukumbuka kuhusu Usalama wa Mwili
Mwili wako ni zawadi kutoka kwa Baba wa Mbinguni. Yeye anataka kukusaidia uwe salama na mwenye furaha. Kama mtu akijaribu kukudhuru kwa maneno au vitendo, hiyo sio SAWA! Tunapaswa kuwa wakarimu na wenye heshima kwa wengine, na tunapaswa tuwategemee wao kuwa wakarimu na wenye heshima kwetu pia.
-
Ni SAWA kusema hapana, hata kwa mtu mzima. Unawajibika kusimamia mwili wako. Hiyo inamaanisha kuamua ikiwa mtu anaweza kukugusa, kukukumbatia au kukubusu. Unaweza kufanya mazoezi ya kusema “Hapana,” “Usiniguse” na “Niache peke yangu.” Ikiwa unaguswa au kuombwa kufanya kitu ambacho kinakufanya usiwe na raha, ni SAWA kusema hapana na kuondoka kama unaweza.
-
Jua ni mguso upi ni salama au hauko salama. Mguso salama unakusaidia kuhisi unapendwa (kama kumbatio au kugonga mikono) au kukaa msafi na mwenye afya (kama mzazi anayekusaidia kuoga au daktari akikusaidia unapokuwa mgonjwa). Wakati mwingine mguso salama unaweza kuumiza, kama kuchoma sindano, lakini ni salama kwa sababu inakufanya uwe na afya. Mguso usio salama unaumiza mwili wako au hisia zako, kama kupigwa, kusukumwa au kugusa sehemu za siri za mtu fulani. Miguso hii yenye maumivu au miguso isiyo furahisha haiko SAWA.
-
Kuna sehemu za mwili wako ambazo ni za siri ambapo mtu mwingine hapaswi kukugusa. Sehemu za siri ni pamoja na sehemu za mwili wako zilizofunikwa na suti ya kuogelea. Si SAWA kwa wengine kugusa sehemu zako za siri (iwe chini au juu ya nguo zako) au kukuomba uguse sehemu zao. Ikiwa hili litakutokea, zungumza kwa mtu mzima wa kuaminika haraka iwezekanavyo.
-
Kumbuka tofauti kati ya siri na mshangao. Mshangao ni kitu cha furaha ambacho kinafurahisha kwa kila mtu, kama zawadi ya siku ya kuzaliwa. Siri ni wakati mtu anapokuambia usimwambie mtu yeyote. Ikiwa umeombwa kuweka siri kuhusu mtu anayekugusa au kukuumiza, unapaswa kumwambia mtu unayemwamini mara moja. Endelea kuwaambia watu wazima wa kuaminika mpaka mtu anapokusaidia kuwa salama.
-
Kama mtu anakugusa au kukuumiza, si kosa lako. Mtu ambaye amekuumiza anaweza kujaribu kukufanya wewe au wengine waamini kwamba ulifanya kosa, lakini hukufanya hivyo. Baba yako wa Mbinguni na Yesu Kristo wanakujua na wanakupenda kiukamilifu. Muombe mtu mzima anayeaminika kwa ajili ya msaada, na kumbuka kwamba daima unaweza kuomba kwa Baba wa Mbinguni kwa ajili ya msaada pia.
Vielelezo na Mike Mullan