“Kadi za Mahekalu,” Rafiki, Septemba 2025, 12.
Kadi za Mahekalu
Hekalu la Mexico City Mexico
-
Hili lilikuwa hekalu la kwanza kujengwa huko Mexico.
-
Sanamu ya malaika Moroni kwenye hekalu hili inashikilia mabamba ya dhahabu.
-
Hili ni hekalu kubwa zaidi nje ya Marekani.
Hekalu la San Juan Puerto Rico
-
Hili lilikuwa hekalu la kwanza kujengwa huko Puerto Rico.
-
Sanaa yake ya kioo inaonyesha uzuri wa kisiwa hicho.
-
Rais Nelson alitembelea kabla ya kutangaza hekalu na kuwaambia waumini kuweka imani yao imara.
Hekalu la Suva Fiji
-
Hekalu hili ni nusu tu ya maili (0.8 km) kutoka baharini.
-
Usanifu katika hekalu ulivuviwa na maua ya Fiji, fukwe na misitu.
-
Wakati wa kuweka wakfu upya mwaka 2016, vijana walitumbuiza kusherehekea waanzilishi wa mwanzo kutoka Pasifiki.
Vielelezo na Rachel Erickson