2025
Shati la Harvey la Ubatizo
Mei 2025


“Shati la Ubatizo la Harvey,” Rafiki, Septemba 2025, 36–37.

Shati la Ubatizo la Harvey

Harvey hakuweza kupata shati lake jeupe mahali popote!

Hadithi ya kweli kutoka Indonesia.

Mvulana na wazazi wake wamekaa nyuma ya teksi

Harvey aliketi nyuma ya teksi pamoja na Ibu (Mama) na Bapak (Baba). Walikuwa njiani kuelekea kanisani kwa ajili ya ubatizo wa Harvey.

“Bapak,ulihisije wakati ulipokuwa unabatizwa? Harvey aliuliza. Bapak alibatizwa miezi michache iliyopita. Sasa kwa vile Harvey alikuwa na miaka minane, alikuwa anaenda kubatizwa pia!

Bapak aliwaza kwa dakika moja. “Maji yalikuwa ya baridi sana!” alisema kwa kicheko. “Lakini pia nilihisi upendo mwingi. Japokuwa wengi wa familia yetu si waumini wa kanisa letu, nilihisi upendo wao na upendo wa Mungu.”

Walipofika kwenye jengo la kanisa, baadhi ya watu kutoka kanisani waliwasaidia kujaza maji kisima cha ubatizo na kujitayarisha.

Mvulana mwenye dhiki akiangalia ndani ya mfuko mtupu; mvulana amevalia shati jeupe ambalo ni kubwa sana

“Harvey, ni wakati wa kubadilisha na kuvaa nguo zako za ubatizo,” Ibu alisema. Harvey alitikisa kichwa na kuupata mfuko wa nguo zake. Lakini nguo zake nyeupe za ndani pekee ndio zilikuwa kwenye mfuko. Hakuweza kupata shati lake jeupe! Alikagua mifuko mingine na kuangalia kuzunguka kanisa.

“Ibu, shati langu halipo hapa,” Harvey alisema.

Ibu alinuna. Alikagua mifuko michache pia. “Lazima tuliliacha ndani ya teksi.”

“Tuna nguo za ziada za ubatizo ndani ya kabati,” Dada Putri alisema. “Nitakwenda kuzichukuwa.”

Lakini nguo pekee za ubatizo kutoka kwenye kabati zilikuwa kubwa mno kwa Harvey. Ibu alionekana mwenye wasiwasi. Ubatizo ungeanza hivi karibuni. Watu wengi walikuwa tayari hapa na Harvey hakuwa na shati lake.

“Labda tunaweza kusema sala ambayo dereva wa teksi atarudisha shati,” Harvey alisema. “Lakini kama hatalileta, ninaweza tu kuvaa shati ambalo ni kubwa sana. Sijali nini nitakachovaa. Nataka tuu kubatizwa”.

Mama na mvulana wakisali

Ibu na Bapak waliitikia kwa kutikisa vichwa vyao. Pamoja walikwenda jikoni, ambako kulikuwa kimya. Kisha wakakunja mikono yao na kuinamisha vichwa vyao.

Harvey alisema sala. “Baba Mpendwa wa Mbinguni , tuna kushukuru kwamba ninaweza kubatizwa leo. Tafadhali msaidie dereva wa teksi kurudisha shati langu. Lakini kama sivyo, ni SAWA pia.”

Baada ya sala yao, Harvey alienda kubadilika katika shati ambalo lilikuwa kubwa sana. Lilishuka mpaka magotini mwake.

“Harvey!” Dada Putri aliita kutoka ukumbini. “Dereva wa teksi yuko hapa.”

Mwanaume akiwa amebeba shati dogo jeupe kwenye henga

Harvey na Ibu walikutana na dereva wa teksi kwenye mlango wa mbele. Alikuwa ameshikilia shati la Harvey!

“Niliangalia nyuma na kuliona kwenye kiti,” alisema. “Nilifikiri linaweza kuwa la kwako.”

“Asante sana, ”Ibu alisema

Harvey alichukua shati kutoka kwa mtu yule. “Asante.”

Mtu yule alitabasamu na kupunga mkono wa kwa heri.

Punde ilikuwa muda wa ubatizo kuanza. Harvey alibadilisha na kuvaa shati lake. Linamkaa kikamilifu! Na lilikuwa jeupe na safi.

Mwanamume akimbatiza mvulana

Wakati Harvey alipoingia ndani ya kisima, maji yalikuwa yanaganda! Bapak alisema sala na akambatiza Harvey. Alipotoka nje ya maji, alihisi safi na mtulivu ndani.

Bapak alimwongoza Harvey nje ya kisima na kufunga taulo laini kuzunguka mabega ya Harvey. Harvey alifikiria kuhusu watu wote waliomsaidia na kumuunga mkono. Ibu, Bapak, dereva wa teksi na familia yake. Na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo pia.

Harvey alimpa Bapak kumbatio. “Uko sawa. Maji yalikuwa baridi!”. Wote wawili walicheka. Kisha Harvey alitazama machoni mwa Bapak. “Lakini ulikuwa sahihi kuhusu kitu kingine pia. Ninahisi upendo mwingi.”

PDF ya hadithi

Vielelezo na Bethany Stancliffe