2025
Mikate Mitano na Samaki Wawili
Mei 2025


“Mikate Mitano na Samaki Wawili,” Rafiki, Septemba 2025, 2–3.

Kutoka Urais wa Watoto

Mikate Mitano na Samaki Wawili

Kutoka kwenye usaili na Lucy Stevenson Ewell.

Yesu Kristo akiwa ameshikilia vikapu vya mkate na samaki, na watu wengi nyuma yake

Mojawapo ya hadithi nizipendazo ni katika Agano Jipya. Zaidi ya watu elfu tano walimsikiliza Mwokozi akifundisha siku nzima. Walianza kupata njaa.

Mmoja wa wanafunzi alisema, “Yupo hapa mtoto, ambaye ana mikate mitano ya shayiri na samaki wawili, lakini hivi ni nini kwa watu wengi kama hawa?” (Yohana 6:9).

Yesu aliwaomba walete chakula Kwake, na Alisali. Ndipo muujiza ukatokea. Kulikuwa na vya kutosha kumlisha kila mtu. Na kulikuwa na vikapu 12 vya mikate vilivyoachwa!

Nawataka mkumbuke ni nani aliyeleta mikate na samaki. Ilikuwa ni mvulana mdogo! Alitoa vyote alivyokuwa navyo kwa Mwokozi.

Watoto ni muhimu sana kwa Baba wa Mbinguni. Unapomfuata Yesu Kristo kwa kuwatumikia wengine, Yeye atakubariki.

Nawe Unaweza Kutoa Pia!

Chora picha ya jinsi unavyoweza kuwatumikia wengine.

Ukurasa wa PDF