“Mihtasari ya Mkutano Mkuu,” Rafiki, Nov. 2025, 4–5.
Mihtasari ya Mkutano
Injili ni Kuhusu Familia
Rais Oaks alifundisha kwamba familia ni kitovu cha injili ya Yesu Kristo. Alipokuwa mvulana mdogo, baba yake alifariki. Lakini mama yake alimfundisha injili, na ilimpa tumaini na amani. Familia zinakabiliwa na changamoto, lakini sote tunaweza kuwa na tumaini kwamba tunaweza kuwa sehemu ya familia ya milele.
Chora picha ya familia yako.
Kufanya Mambo Magumu pamoja na Kristo
Mzee Eyring alisema kwamba alipokuwa chuoni, fizikia na hisabati zilikuwa ngumu kwake. Alihisi kuzidiwa na alitaka kuacha. Aliposali, alihisi kufarijiwa na kutiwa moyo. Alijifunza kwamba angeweza kufanya mambo yote katika Kristo, ambaye anatuimarisha sote (ona Wafilipi 4:13). Tunapokabiliana na nyakati ngumu, Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo watakuwa pamoja nasi.
Chora au andika kuhusu wakati ulipofanya jambo gumu kwa msaada wa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Mkweli kwenye Ushuhuda Wako
Mzee Brown alishiriki kwamba alijiunga na Kanisa huko Jamaica. Marafiki zake walimwuliza, “Unawezaje kujiunga na kanisa hilo? Je, kweli unaamini hayo yote?” Lakini alikuwa amepata ushuhuda kutoka kwa Roho Mtakatifu, na alibaki mkweli kwa ushuhuda wake. Tunapochagua kuamini, shuhuda zetu zitakua.
Chumba kwa ajili ya Nabii
Dada Spannaus alisimulia hadithi ya Biblia kuhusu mwanamke aliyemwalika nabii Elisha ili akale nyumbani kwake. Mwanamke hata alijenga chumba ndani ya nyumba yake ili aweze kuwa na mahali pa kukaa. Roho Mtakatifu alimthibitshia kwamba Elisha alikuwa nabii wa Mungu. Sisi pia tunaweza kuwa na ushuhuda juu ya manabii wa Mungu. Tunaweza kufungua mioyo yetu na kutii maelekezo yao.
Nguvu ya Nyimbo za Msingi
Dada Browning alizungumza kuhusu umuhimu wa nyimbo za Msingi. Alisema kwamba muziki ni chombo ambacho kinaweza kusaidia kupanda mbegu za ushuhuda katika mioyo yetu. Tunapoimba nyimbo za Msingi, tunaimba shuhuda zetu za injili ya urejesho. Yesu kweli anatutaka tuwe miale ya jua!
King of Love, My Shepherd by Julie Rogers. May not be copied.