2025
Shughuli za Njoo, Unifuate
Novemba 2025 Rafiki


“Shughuli zaNjoo, Unifuate ,” Rafiki, Novemba 2025, 22–23.

Shughuli za Njoo, Unifuate

Oktoba 27–Novemba 2: Mafundisho na Maagano 124

Mioyo ya Uadilifu

Watoto wawili wakipaka rangi mioyo kwenye karatasi

Bwana alimpenda mtumishi Wake Hyrum Smith kwa sababu ya “uadilifu wa moyo wake” (Mafundisho na Maagano 124:15). Tafuta neno uadilifu linamaanisha nini na zungumza kuhusu hilo na familia yako. Kisha chora moyo mkubwa kwenye kipande cha karatasi. Ndani ya moyo, chora au andika kitu unachoweza kufanya ili kuwa na uadilifu.

Novemba 3–9: Mafundisho na Maagano 125–128

Fremu ya Picha ya Familia

Wakati Brigham Young aliporudi kutoka misheni yake, Bwana alimwamuru kutunza familia yake (ona Mafundisho na Maagano 126). Tengeneza na upambe fremu ili kuweka picha ya familia yako. Ni kwa jinsi gani unaweza kujaliana?

Novemba 10–16: Mafundisho na Maagano 129–132

Kumfuata Kiongozi

Watoto wawili wakipapasa vichwa vyao

Miili yetu ni kama miili ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo (ona Mafundisho na Maagano 130:22). Cheza mchezo huu ili kusherehekea mwili wako! Fanya zamu kuchagua kitendo, kama vile kuruka au kupapasa kichwa chako. Kila mtu mwingine anaiga kitendo hicho.

Novemba 17–23: Mafundisho na Maagano 133–134

Huduma ya Upendo

Yesu Kristo ni mwenye upendo na mkarimu (ona Mafundisho na Maagano 133:52). Weka jina la kila mtu katika bakuli. Chagua jina na kwa siri mhudumie mtu huyo wiki hii.

Novemba 24–30: Mafundisho na Maagano 135–136

Hadithi ya Joseph Smith

Mvulana akipaka rangi picha

Joseph Smith alikuwa Nabii wa Urejesho (ona Mafundisho na Maagano 135:3). Chora picha kutoka kwenye maisha yake. Ni kwa jinsi gani wewe unaweza kujua yeye alikuwa ni nabii?

Ukurasa wa PDF

Picha na Christina Smith