2025
Kujifunza kutoka kwenye Mkutano Mkuu
Novemba 2025 Rafiki


“Kujifunza kutoka kwenye Mkutano Mkuu,” Rafiki, Novemba 2025, 6-7.

Kujifunza kutoka kwenye Mkutano Mkuu

Maelezo ya Mapishi ya Habari Njema

Mzee John D. Amosi alitufundisha kufuata maelezo ya mapishi ya Mungu katika maandiko kwa ajili ya kuishi kwa furaha. Tazama kila andiko ili kuona ni viungo gani vinamwalika Yesu Kristo katika maisha yako. Chora mishale ili kuiongeza kwenye chungu cha jambalaya. Weka X juu ya viungo usivyopaswa kutumia.

Kusikiliza Mkutano Mkuu

Daima natazamia mkutano mkuu. Kusikiliza mafundisho ya Mitume na nabii wetu daima hunifanya niwe na furaha. Pia ninashiriki mafundisho na kaka yangu na majirani zangu. Mafundisho yananikumbusha kwamba Mungu ananipenda kila siku.

Jianna A., umri miaka 9, Wilaya ya Kisumu, Kenya

Ninapenda mkutano mkuu. Daima tunatazama kwenye TV.

Ismael R., umri miaka 8, Idara ya Lima, Peru

Kusherehekea Tangazo la Familia

Mkutano huu ulikuwa unaadhimisha miaka 30 ya “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu.” Rais Dallin H. Oaks alituhimiza kutumia muda kufanya mambo mazuri na familia zetu. Ni baadhi ya mambo gani unaweza kufanya pamoja na familia yako? Yaandike kwenye kadi hapa chini. Kisha kata kadi ili ikusaidie wewe kukumbuka mawazo yako!.

Page PDF with illustration of girl making jambalaya

Illustrations by Josh Talbot