“Kwa Ajili ya Watoto Wakubwa,” Rafiki, Novemba 2025, 34–35.
Kwa Ajili ya Watoto Wakubwa
Maneno kutoka Kwako
Nilijifunza kuhusu nabii Samweli kanisani, na ninaipenda hadithi hiyo!
Liam F., miaka 9, Okinawa, Japani
Ninajua kwamba Yesu Kristo ananijua na anajua mimi ni nani. Ninamshukuru Yeye kwa kunifariji katika wakati mgumu na kwa kutoniruhusu nipitie haya pekee yangu.
Antonella D., miaka 10, Rio Grande do Sul, Brazili
Historia ya Familia Ukurasa wa Vichekesho
Andika au chora hadithi ya kweli kwenye visanduku hapo chini: Ungeweza kushiriki hadithi kutoka kwenye historia ya familia yako au wakati ambapo ulichagua kilicho sahihi. Tutumie picha utakapomaliza! Nenda kwenye jalada la nyuma ili uone jinsi kutuma.
Fumbua Msimbo
Zaka ni baraka! Fedha za zaka husaidia Kanisa kujenga mahekalu na makanisa, kuchapisha maandiko, kuwasaidia wamisionari, na mengine mengi zaidi. Tunapotii amri ya kulipa zaka, Baba wa Mbinguni hutubariki katika njia nyingi (ona Malaki 3:10).
Tambua thamani ya kila sarafu. Kisha tatua fumbo la mwisho. Ni kiasi gani cha zaka unapaswa kulipa? (Dokezo: zaka ni asilimia 10.)
Vielelezo na Josh Talbot