2025
Nini Hutokea Wakati Nabii Anapofariki?
Novemba 2025 Rafiki


“Nini Hutokea Wakati Nabii Anapofariki?” Rafiki Oktoba 2025, 3–45.

Nini Hutokea Wakati Nabii Anapofariki?

  1. Bwana huwaita manabii kuongoza Kanisa Lake, na Yeye ana mpango kwa ajili ya wakati ambapo mmoja wao anafariki. Yeye daima huliongoza na kulielekeza Kanisa Lake!

  2. Wakati Rais wa Kanisa anapofariki, Akidi ya Mitume Kumi na Wawili inaliongoza Kanisa. Hii sasa inajumuisha Mitume wawili ambao walikuwa washauri katika Urais wa Kwanza.

  3. Mitume husali na kuamua lini waunde Urais mpya wa Kwanza.

  4. Bwana anamwita Mtume aliye hudumu kwa muda mrefu zaidi ili kuwa nabii anayefuata na Rais wa Kanisa.

  5. Kupitia nabii mpya, Bwana huwaita Mitume wawili kama washauri katika Urais mpya wa Kwanza.

  6. Mtume mpya ataitwa kuhudumu katika Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

  7. Wakati wa mkutano mkuu, tunainua mikono yetu kuukubali Urais mpya wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Kuwakubali inamaanisha tunakubali kuwapenda na kuwasaidia na kufuata mwongozo wao kama watumishi wa Bwana.

  8. Wakati Rais mpya wa Kanisa au Mtume anapoitwa, unaweza kusali ili kujua kwamba waliitwa na Mungu. Na unaweza kuwakubali na kuwasaidia kwa kusikiliza maneno yao na kuwafuata!

Page PDF