“Joseph Anafariki kwa ajili ya Injili,” Rafiki, Novemba 2025, 26–28.
Hadithi za Maandiko
Joseph Anafariki kwa ajili ya Injili
Watu wengi walikasirishwa na Joseph Smith na Kanisa. Hawakupenda kile Jpseph alichokuwa akifundisha. Baadhi ya watu hata walitaka kumuua.
Joseph alipaswa kwenda katika mji wa Carthage ili hakimu aweze kuamua kama alikuwa amevunja sheria. Joseph alimbariki Emma na watoto wake, akawabusu akiwaaga, na akaondoka kwenda Carthage.
Hyrum, kaka yake Joseph na marafiki wengine walikwenda pamoja naye. Walipokuwa wakiondoka, Joseph alitazama nyuma huko Nauvoo. “Hapa ni mahali pa kupendeza zaidi na watu bora chini ya mbingu,” alisema.
Katika Carthage wanaume hawa waliwekwa jela. Hyrum aliwasomea kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni. Joseph aliwaambia walinzi kwamba Kitabu cha Mormon ni cha kweli.
Baadaye siku hiyo, wanaume wenye hasira wakiwa na bunduki walikimbia haraka na kuingia jela. Walianza kupiga risasi ndani ya chumba ambamo Joseph na marafiki zake walikuwemo. Hyrum na Joseph waliuawa.
Watakatifu walikuwa na huzuni sana walipogundua kwamba Joseph na Hyrum walikuwa wamefariki. Lakini walijua kwamba Kanisa lingeendelea kukua na kuwabariki watoto wa Mungu ulimwenguni kote.