2025
Kumfuata Yesu huko Uhispania
Novemba 2025 Rafiki


“Kumfuata Yesu huko Uhispania,” Rafiki, Novemba. 2025, 14–15.

Kumfuata Yesu huko Uhispania

Kutana na Eimy

Msichana mwenye tabasamu pamoja na familia yake

Eimy anamfuata Yesu Kristo kwa kuisaidia familia yake na kucheza na binamu zake. “Ninapowahudumia wengine, ninahisi vizuri sana na mwenye furaha,” anasema.

Eimy pia anashiriki kuhusu Kanisa na wengine. “Nilihisi furaha sana niliposhiriki injili pamoja na rafiki zangu shuleni,” anasema. Alimwalika mmoja wa marafiki zake kwenye ubatizo wake na kusali kwa ajili yake. Pia anapenda kushiriki chakula chake na wanasesere wake pamoja na wengine.

Kuhusu Eimy

Msichana mwenye tabasamu akiwa na maua ya rangi ya waridi

Umri: miaka 8

Kutoka: Guadalajara, Uhispania

Lugha: Kihispania

Lengo: Kwenda kutembelee familia yake huko Colombia

Mambo apendayo: Sarakasi, kwenda sinema na familia yake, na kucheza katika uwanja wa burudani na rafiki zake

Familia: Eimy, kaka wawili, Mama, na Baba

Msichana na wavulana wawili wakicheza nje

Mapendeleo ya Eimy

Hadithi ya Maandiko: Wakati Yesu Kristo alipowafundisha watoto

Chakula: Arepas (mkate uliojazwa)

Tunda na mboga: Ndizi na saladi

Rangi: Waridi, zambarau, kijani

Wimbo wa Msingi:I Am a Child of God” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2)