2025
Kutazamia Programu ya Vijana
Novemba 2025 Rafiki


“Kutazamia Programu ya Vijana,” Rafiki, Novemba 2025, 38–39.

Kutazamia Programu ya Vijana

Kuondoka kwenye Msingi mwaka unaofikia miaka 12 wakati mwingine kunaweza kuonekana kama kunaogopesha au hata kuhuzunisha. Kwa bahati nzuri, kuna mambo mengi ya kusisimua kuhusu kutimiza miaka 12 na kujiunga na darasa lako la Wasichana au akidi ya Ukuhani wa Haruni! Hizi chache ni baadhi tu.

1

Hekalu

Unaweza kukutana na askofu wako ili kupata kibali cha hekaluni na kufanya ubatizo kwa niaba ya wafu hekaluni!

2

Shughuli na Matukio

Utakuwa na shughuli nyingi pamoja na kikundi chako cha Wasichana au kikundi cha Ukuhani wa Haruni. Unaweza pia kwenda kwenye kambi za vijana ili kuwa na burudani na wengine wakati ukijifunza kuhusu Yesu Kristo na injili Yake!

3

Hudumu Kanisani

Unaweza kupata wito wa kuhudumu katika urais wa darasa au akidi. Pia utakuwa na fursa za kufundisha darasa lako, kusaidia kupanga shughuli, na kuhudumu katika njia zingine!

4

Mikutano ya Seminari na KNV

Katika mwaka unapofikia umri wa miaka 14, unaweza kuanza kuhudhuria seminari ili kujifunza zaidi kuhusu Yesu Kristo na injili Yake ya urejesho. Unaweza pia kuhudhuria mikutano ya KNV (Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana) pamoja na vijana wengine wanaompenda na wanataka kumfuata Yesu Kristo.

5

Maudhui Mapya kwa ajili Yako!

  • Kwa msaada wa mzazi, agiza jarida la Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana kwenye tovuti ya Kanisa.

  • Mwombe mzazi kuhusu kupakua Aplikesheni ya Kuishi Injili. Ina mawazo ya kuburudisha kwa ajili ya kujifunza injili na kuweka malengo kwa ajili ya programu ya Watoto na Vijana.

  • Jisomee Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi Kijitabu hiki kiliandikwa ili kukusaidia wewe kumfuata Yesu Kristo.

  • Wewe na familia yako mnaweza kupata hadithi za kuinua, muziki, matangazo, na zaidi kwenye akaunti za Strive to Bee za mitandao ya kijamii.

Ukurasa wa PDF wa wavulana na wasichana wakifanya shughuli tofauti