2025
Tayari Kuendelea Kukua
Novemba 2025 Rafiki


“Tayari Kuendelea Kukua,” Rafiki, Novemba 2025, 36–37.

Tayari Kuendelea Kukua

Jewel hakutaka kuwaacha marafiki zake katika Msingi!

Hadithi ya kweli kutoka Palau.

Jewel aliketi kwenye benchi katika mkutano wa sakramenti pamoja na wazazi na kaka yake. Alichora picha za hadithi za maandiko. Alijaribu kumsikiliza mzungumzaji, lakini tumbo lake lilihisi kama lilikuwa limejaa vipepeo wa wasiwasi!

Leo ilikuwa siku ya kwanza ya Jewel kwenda darasa la Wasichana badala ya Msingi. Hakutaka kuwaacha nyuma marafiki zake katika Msingi. Alipenda kuimba na kusoma maandiko pamoja nao.

Lakini Jewel alikuwa akifikia umri wa miaka 12 mwaka huu. Ulikuwa wakati wa kuhamia kwenye programu ya Wasichana.

Jewel alifunga macho yake na kusema sala ya kimya kimya. Baba wa Mbinguni, tafadhali nisaidie kuwa na darasa zuri la Wasichana.

Baada ya sala ya kufunga katika mkutano wa sakramenti, Jewel alivuta pumzi ndefu na kutembea kwenda darasani. Wasichana wakubwa tayari walikuwa pale. Kulikuwa na wanne kati yao. Walikuwa wakiongea na kucheka cheka.

“Mambo,” Jewel alisema.

Walitabasamu. “Hujambo.”

Mwalimu aliingiai na kumkaribisha Jewel. Kisha akaanza somo.

Kwa muda mwingi wa darasa, Jewel alijisikia mpweke. Alikuwa na wasiwasi kuzungumza kwa sababu hakuwajua wasichana wengine bado. Angepaswa kuwa katika darasa la Wasichana kwa muda mrefu. Ilihisi kama ni milele. Je, daima angejisikia mpweke hapa?

Kisha sauti ndogo likamjia akilini mwake. Hutakuwa katika Darasa la Wasichana milele. Umekuwa tu mkubwa vya kutosha kuendelea na kujifunza zaidi kuhusu kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo.

Jeweli alihisi kufarijiwa na maneno haya. Aliyatambua maneno yale kama Roho Mtakatifu alikuwa akimsaidia yeye. Ingawa hakuwa na marafiki wengi katika darasa la Wasichana bado, hakuwa peke yake. Alikuwa na Roho Mtakatifu.

Baada ya darasa kumalizika, Jewel aliitafuta familia yake.

“Darasa la Wasichana lilikuwaje?” Mama aliuliza.

Jewel alimpa kumbatio. “Lilikuwa SAWA!” Ninakosa Msingi, na bado sijawajua wasichana wale . Lakini nilimhisi Roho Mtakatifu akinifariji.”

Mama alitabasamu. “Hiyo ni vizuri kusikia! Na pengine wakati ujao utakuwa bora zaidi.

Jewel alitikisa kichwa. Alitumaini Mama alikuwa sahihi.

Wakati mwingine alipokuwa na darasa la Wasichana, Jewel alisema salamu kwa wasichana tena.

“Jambo Jewel,” mmoja wao alisema. “Unapaswa kukaa karibu nami!”

Jewel alitabasamu na kuketi karibu na msichana yule. Jina lake lilikuwa Ellie. Waliongea sana kabla ya somo kuanza. Ellie alikuwa mkarimu na alimfanya ajisikie kukaribishwa.

Msichana katika darasa la Wasichana akiinua mkono wake, wasichana wengine wawili wanatazama

Wakati wa somo, mwalimu aliuliza kama mtu ye yote alikuwa na uzoefu na Roho Mtakatifu.

Jewel aliinua mkono wake. “Nilihisi Roho Mtakatifu akinisaidia nilipokuwa na wasiwasi kujiunga na Wasichana,” alisema. “Roho Mtakatifu hunisaidia ninapokua na kukabiliana na changamoto.”

Jewel alikuwa akifikiria jinsi Roho Mtakatifu alivyomfariji alipohisi mpweke. Ilionekana vizuri kushiriki uzoefu wake na wasichana katika darasa la Wasichana.

Baada ya kushiriki, wasichana wengine wachache walishiriki pia. Jewel alipenda kusikia kile walichosema.

Jewel bado alikosa darasa la Msingi wakati mwingine. Lakini kwa sababu ya Roho Mtakatifu, alikuwa tayari kuendelea kukua.

PDF ya hadithi

Kielelezo na Liz Brizzi