2025
Maneno Yangu ya Injili
Novemba 2025 Rafiki


“Maneno Yangu ya Injili,” Rafiki, Novemba 2025, 10.

Maneno Yangu ya Injili

Tafuta maneno haya na virai katika toleo hili la jarida la Rafiki!

Zaka

Kielelezo cha hekalu na fedha kutoka nchi tofauti

Kulipa zaka ni kurudisha kwa Baba wa Mbinguni kwa kuchangia sehemu moja ya kumi (asilimia 10) ya pesa tunazopata kwa Kanisa Lake. Zaka husaidia kujenga mahekalu na makanisa na kusaidia kazi ya Kanisa. Tunapolipa zaka, Baba wa Mbinguni hutubariki katika njia nyingi!

Mababu

Kielelezo cha nembo ya FamilySearch ya mtindo wa mti wa familia

Mababu zetu ni watu katika familia yetu ambao waliishi muda mrefu uliopita, kama babu na bibi wakuu wetu. Mababu ni sehemu muhimu ya historia ya familia yetu. Tunaweza kujifunza kuwahusu wao, kuwakumbuka, na kufanya kazi ya hekaluni kwa niaba yao ili tuweze kuwa pamoja nao milele.

Farahisisha

Kufarahisisha ni njia tunayoweza kuwasaidia wengine kuwapata mababu wao! Tunaandika majina kutoka kwenye kumbukumbu za zamani za karatasi kwenye kompyuta ili watu waweze kuwatafuta wanafamilia wao na kupata kumbukumbu kuhusu maisha yao. Hii inasaidia kwenye historia ya familia na kazi ya hekalu ili watu wengi zaidi waweze kuunganishwa pamoja milele. Hata watoto wanaweza kusaidia kwenye kufarahisisha!

Kifo cha kishahidi

Kifo cha kishahidi hutokea wakati mtu anapokufa kwa ajili ya kitu wanachoamini. Joseph Smith na kaka yake Hyrum walikuwa wafia dini kwa sababu waliuawa kwa ajili ya walichoamini, walichoishi, na kufundisha injili ya urejesho ya Yesu Kristo.

Ukurasa wa PDF

Vielelezo na Madison Baker